Goli
pekee la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC, limeipa ushindi
timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya SOFAPAKA uliochezwa jana
Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya.
Azam FC imecheza mchezo wake wa pili wa kirafiki, juzi jioni walifungwa 2-1 na AFC Leopard katika mechi iliyochezwa uwanja huo.
Katika
mchezo huo, kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka
suluhu, wachezaji wa Azam FC Himid Mao alipiga mpira wa adhabu uliogonga
mwamba na kurudi ndani katika dakika ya 14, dk 22 Seif Abdalah akiwa na
lango la SOFAPAKA alipiga mpira uliotoka nje.
Azam
FC waliendelea kufanya amshambulizi katika lango la SOFAPAKA, dk 27 na
45 Michael Bolou alipiga shuti likatoka nje na dakika ya 37 Humprey
Mieno alishindwa kufunga na badala yake shuti likaokolewa na kipa wa
SOFAPAKA, Duncan Ochieng
SOFAPAKA
dk 24 Kago Dawson alikosa nafasi ya wazi kwa kupiga shuti lililodakwa
vyema na kipa chipukizi wa Azam FC, Aishi Salum ambaye aliweza kulinda
lango hilo katika vipindi vyote.
Kipindi
cha pili Azam FC walifanya mabadiliko walitoka Samih Haji Nuhu, Michael
Bolou, Khamis Mcha na David Mwantika nafasi zao zikachukuliwa Luckson
Kakolaki, Abdulhalim Humud, Gaudence Mwaikimba na Malika
Ndeule,mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi hicho na kufanya mashambulizi
mengi.
Kipa
Aishi Salum alitumia vema nafasi aliyoipata katika mchezo huo kwa
kuzuia mashuti ya wachezaji wa SOFAPAKA na kusimama vema katika nafasi
hiyo, kutokana na umri wake mdogo amecheza katika kiwango cha juu kama
anavyokuwa golikipa namba moja Mwadini Ally ambaye jana alipumzishwa na
kuwapisha vijana Aishi na Jackson Wandwi.
Azam
FC walipata goli katika dakika ya 58 kupitia kwa mkwaju wa penati
iliyopigwa na Mwaikimba baada ya beki wa SOFAPAKA Kisuya Colins kunawa
mpira katika eneo la hatari.
Goli hilo lilidumu hadi
kumalizika kwa mchezo huo na kuifanya Azam FC kushinda 1-0 katika
mchezo huo ulioshuhudiwa na Raisi wa SOFAPAKA, Elly Kalekwa na Katibu
Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa.
Azam
FC kesho itapumzika na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa City ambao
watacheza siku ya Jumanne dhidi ya K.C.B na kumalizia safari hiyo ya
mechi za kirafiki ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya ligi kuu na
Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam
FC, Aishi Salum, Himid Mao/Omary Mtaki, Samih Haji Nuhu/Luckson
Kakolaki, Jockins Atudo, David Mwantika/Malika Ndeule 45’, Michael
Bolou/Abdulhalim Humud 45’, Humphrey Mieno/Ibrahim Mwaipopo 66’, Salum
Abibakar, Brian Umony Jabir Aziz 81’, Seif Abdalah/Uhuru seleman 68’,
Khamis Mcha/ Gaudence Mwaikimba.
SOFAPAKA
Duncan Ochieng/Okeko David, Shivash Collins, Kisuya Collins, Situma
James, Felly Mulumba, Abdalah Nyanzi, Hilary Echesa, Koko Manopi, Kagogo
Patrick/George Owino, Kago Dawson na John Baraza/Tarumbwa Cabadian
Post a Comment