WAZIRI
wa Chakula na Ushirika, Christopher Chiza amewagiza wakuu wa mikoa
kutumia madaraka waliyonayo kwa kuwachukulia hatua za kisheria mawakala
watakaouza unga kinyume na bei elekezi ya sh 750 hadi 900 kwa kila
kilo.
Chiza
alisema hao wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari jijini
Dar es Salaam kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini.
Alisema
serikali imeidhinisha kuuzwa tani 40,000 za mahindi kwa mawakala,
kutoka katika ghara la chakula la taifa kwa ajili ya maeneo yenye
upungufu wa chakula, kwa bei ya sh 450 kwa kila kilo ambapo zoezi hilo
limekwisha anza Januari na litaendelea hadi Machi mwaka huu.
“Lazima
wakuu wa mikoa, wa wilaya, wenyeviti wa mitaa kwa kushirikiana na
wanannchi wenyewe mshirikiane kwa pamoja katika suala zima la kudhibiti
bei ya unga”alisema.
Chiza
alisema mikoa itapaswa kuwachukulia hatua mawakala (sagishaji), ambao
watabainika kuuza unga huo kinyume na bei elekezi ya serikali.
“Mikoa
itachukuwa hatua kwa msagishaji ambaye atabainika kutumia vibaya kibali
alichopewa kama vile kuuza kibali hicho kwa msagishaji mwingine,
kusafirisha na kuuza mahindi au unga kwenye maeneo tofauti aliyopangiwa,
kutosagisha na kuuza unga ndani ya siku saba kwa mujibu wa mkataba”
alisema.
Chiza
aliitaja baadhi mikoa yenye uhaba unga wa mahindi pamoja na tani
walizopatiwa kuwa ni Arusha (tani 1100), Dodoma (400), Kilimanjaro
(400), Lindi (400), Mara (900), Manyara (800).
Mingine
ni Morogoro (400), Mwanza (2500), Shinyanga (1029), Singinda (500),
Tabora (1000), Tanga (700),Mtwara (600), Pwani (700) Simiyu (1971) na
Dar es Salaam (6400).
Post a Comment