Mheshimiwa Jesca Msambatavangu akifurahia siku ya kampeni zake za kuomba udiwani
Hapa Jesca Msambatavangu (kushoto) akitekeleza ahadi zake kwa kikundi cha wajasiriamali.
Ndugu
wananchi katika uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi vya siasa ili kushika
Dola na kuunda Serikali kila Chama huandaa Ilani yake ya Uchaguzi.
Ilani
hutafsiri na kuelezea Sera zake na kuhusu maeneo muhimu ya siasa,
Uchumi na jamii, na hutoa maelezo fasaha kuhusu mikakati ya utekelezaji
wa sera zinazonadiwa pindi wagombea wake wakifanikiwa kushinda.
Hivyo
basi Chama cha Mapinduzi kilishinda na kushika Dola hivyo ilani yake
ndiyo inayotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015.
Mimi
pia ni mmoja kati ya wagombea wa CCM kwa ngazi ya kata yaani Diwani,
katika kata ya Miyomboni Kitanzini ambaye nina wajibu wa kutekeleza
ilani hiyo katika ngazi ya Kata hatimaye jimbo kwa kuungana na madiwani
wengine katika manispaa yetu.
Ifuatayo ni taarifa ya utekezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2010/2012 kwa ngazi ya kata ikiungana na jimbo.
SURA YA KWANZA
MAFANIKIO YA KIUCHUMI NA KIJAMII MIAKA 5 YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE
Katika
sura hii inaelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Serikali ya
awamu ya Nne kipindi cha miaka 5 (2005-2010). Ili lenga katika
kutekeleza kipindi cha pili na cha mwisho cha mwelekeo wa sera za CCM
katika miaka ya 2000-2010. Kwa kuzingatia Dira ya maendeleo ya Taifa ya
2025 na malengo ya millennia.
Inaelezea mafanikio yaliyopatikana, kiuchumi, kijamii na kisiasa.
SURA YA PILI
KUJENGA MSINGI WA UCHUMI WA KISASA WA TAIFA LINALOJITEGEMEA
Mwelekeo
wa sera za CCM katika miaka 2010-2020 umeanisha jukumu kubwa la Nchi
yetu; katika kipindi hiki ni kutekeleza lengo la dira ya maendeleo ya
Taifa 2025 (Tanzania development vision). Ambalo Lengo ni;
“Kuleta Mapinduzi ya Uchumi ulio nyuma na tegemezi na kuingiza katika mkondo wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea”
Ili
kutekeleza dira hii ndiyo maana mwelekeo wa CCM kupitia Ilani;
unaiagiza Serikali kutekeleza majukumu kupitia Ilani yake ambayo
yatalenga kutimiza malengo ya millennia na Dira ya maendeleo ya Taifa.
Ikiwa ni pamoja na kujenga Uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea
yaani modernation ya Uchumi. Kwa kila ngazi, sasa wote pia kwa pamoja
kuanzia ngazi ya mtaa hadi Taifa lazima tutekeleze malengo haya ya dira
ya maendeleo kwa Taifa letu kila mtu kwa nafasi yake.
KILIMO
Kwahiyo
kila sekta kama ni Kilimo wajue lengo ni kujenga Uchumi wa
kisasa utakaopelekea Taifa letu kujitegemea. Wadau ambao ni wakulima,
maafisa ugani au kilimo, wazalishaji wa pembejeo kama mbolea na mbegu,
wauzaji wa pembejeo, vyuo vya mafunzo ya kilimo wote kwa pamoja wajue
tunajenga uchumi wa kisasa utakaopelekea Taifa letu kujitegemea.
Sasa
kama wengine wanazalisha mbegu bora, wauzaji wanachakachuka, wakulima
wanapewa mbegu na mbolea za ruzuku wanauza vocha, Vyuoni hakuna utafiti
wakutosha kusaidia mapinduzi haya ya kilimo ni tatizo katika kufikia
mpango wa maendeleo wa Taifa letu; ambalo tunategemea sisi na watoto
wetu waendelee kuishi humu.
Sasa
basi Ilani hii 2010-2015 inalengo la Kuongeza KASI ya ujenzi wa Uchumi
wa Kisasa na Taifa linalojitegemea kwa kuwashirikisha na kuwawezesha
kiuchumi wananchi.
Kwa vipi?
Kuongeza
maarifa na matumizi ya sayansi na Teknolojia katika sekta za
Uzalishaji. Ili kuongeza Uzalishaji,Ufanisi na Tija au faida katika
uchumi hususani katika:
· Kilimo
3(31-56) -ndipo ikaanzishwa program ya Kilimo kwanza. Ambayo itaelezea
upatikanaji wa Fedha za uwekezaji katika sekta ya Kilimo; Mbegu bora;
Zana za kisasa; Matumizi ya mbolea; Elimu kwa wakulima kuhusu kanuni za
kilimo; huduma za ugani; mikopo kwa wakulima; upatikanaji wa masoko;
utafiti na matokeo; kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.
· Ufugaji – Kubadili wakulima kutoka ufugani duni na kuwa wafugaji bora, sio tu wakuhama hama.
Kutatua
matatizo ya malisho na maji kuwafikisha wafugaji katika ukulima
mchanganyiko na ufugaji wa mabandani, wenye tija kubwa utakao toa nyama
na maziwa bora.
Ili kujenga uchumi wa kisasa na kujitegemea. Ndiyo maana mjini kuna Nyama na maziwa.
Bila mipango hii wale watoto wetu vichanga wangekunywa nini; hizo nyama choma zingekuwepo.
· Uvuvi – Mkazo unalenga katika kuwapatia wavuvi maarifa yatakayobadili na kuongeza uzalishaji wa samaki.
Samaki wakiongezeka wanaonufaika sio wavuvi peke yao kwa kupata faida; lakini pia wauzaji wa samaki na walaji wa samaki.
Mwisho uchumi utaimarika na watu kujitegemea.
Pia
Serikali katika hili, inatilia mkazo uwezeshaji kwa wavuvi, kuendeleza
viwanda vya samaki, na kusimamia uvunaji endelevu wa samaki.
· Viwanda
– Kutoa msukumo katika mapinduzi ya viwanda; kuhamasisha maendeleo ya
Sayansi, teknolojia, na uhandisi, viwanda vya msingi, kati na vidogo.
Ikiwa ni pamoja na kusimamia viwanda ambavyo tunavyo vya watu binafsi na
Serikali.
NB:Mikakati
mbali mbali inatekelezwa kama; MKURABITA, Ushirika, Mfuko wa Pembejeo
za Kilimo, Mifuko ya uwezeshaji,Mfuko wa maendeleo ya Jamii na Benki ya
wanawake.
SURA YA TATU
SEKTA YA UZALISHAJI MALI
KILIMO-3(31-38)
UTANGULIZI
Ndugu
wananchi watu wengine wanabeza swala la kilimo kwanza. Hivi kweli
chakula sio kitu cha kwanza katika Nchi? Unaweza ukafanya cho chote
unachofanya kama haujala? Swali huwa linaulizwa; UNAISHI ILI ULE AU
UNAKULA ILI UISHI? JIBU 1.UNAKULA ili UISHI ndiyo jibu sahihi. 2.Wale
wanaobeza Kilimo kwanza ndiyo ambao wangejibu UNAISHI ili ULE.
Sasa
kama watu wote sisi milioni 44 na kitu lazima tule hata kama ni mlo
mmoja kwa siku, nadhani kilimo ni kwanza.Kuvaa unaweza ukavaa nguo mbili
kwa wiki lakini hauwezi kula ugali ule ambao ulisha kula jana ukatoka
tumboni ukala leo.
Hiyo ndiyo maana kilimo lazima kipewe kipaumbele.
Hata kulala utalala kitanda na nyumba hiyo hiyo kwa miaka mingi lakini sio kula.Na hapo na ufugaji uko ndani yake.
Na
kama kilimo hakitiliwi mkazo inakuwaje ninyi hapa sokoni kila siku
wengine tangu wazazi wenu, tangu utoto mpaka mnazeeka mnauza tu
malimbichi zinatoka wapi?
PEMBEJEO ZA KILIMO-3(32d)
Mbolea
za ruzuku na mbegu bora; zimetolewa na hasa ilikuwa kuwasaidia wale
watu wasio na uwezo kabisa, sio kuwatosheleza kuwasaidia. Kata yetu sisi
kutokana na mazingira yake mbolea hizi tumepewa vocha 59 vipaumbele
tuliwapa vijiji zaidi. Na zimetolewa kwenye mitaa yetu yote.
Tatizo
pia ni uelewa kwamba wapewe wale wasio na uwezo, lakini pia wengine
wanapewa vocha wanaziuza, shambani hatumii tena, wala shamba hana.
Lakini pia kuna mbolea za samadi na mboji watu wanaweza kutumia pia.
Uanzishaji wa uzalishaji wa mbegu bora kupitia majeshi lakini pia, kutoa ruzuku kwenye dawa za mifugo nk.
Sisi
kama Kata ya Miyomboni Kitanzini tunanifaika na kilimo kwanza hasa kwa
sababu tuna masoko yote makubwa hapa, ambayo huuza bidhaa za mashambani,
hivyo kutuimarishia uchumi wetu.
UVUVI-3(39)
Kata
yetu inanufaika na sera hiyo kwani zaidi ya kupata kitowe cha Samaki
lakini kiuchumi ni biashara yetu. Kwa kweli tunaonga mipango endelevu
kwa uhai wa samaki ili tuendelee kufanya biashara ya samaki.
UTALII-3(45)
Utalii
unaendelea kukua katika mji wetu, hata sisi tumeona faida za moja kwa
moja za utalii. Mfano hapa sokoni, soko hili la zamani ni la kihistoria
na lilikuwa soko la kwanza Africa. Ndiyo maana wazungu wanakuja kuja
kula humo ndani kwa akina mama. Akina mama inabidi mjitahidi yes na no
zisiwapige chenga.
Ila
nadhani kuna changamoto ya mlango na maji kutiririka sehemu Fulani na
dhani kina mama waseme vizuri ili tuone namna ya kuboresha.
Lakini
sisi kata yetu ina hivyo vitu viwili vya kihistoria kama vivutio vya
utalii, ambalo hili soko na Eneo la Kitanzini ambapo walikuwa
wananyongewa watu. Na manispaa imeshaanda mpango wa kupaendeleza ili
kutunza kumbu kumbu hiyo, pamoja na vingine vilivyo ndani ya manispaa.
SURA YA NNE
ARDHI-4(57-59)
Ardhi
ni raslimali muhimu katika kuchangia maendeleo. Ina umuhimu kabla na
hata baada yakuendelezwa ili mradi tu ikithaminishwa na kutambulika
kisheria uthamani wake.
Upimaji wa Viwanja/maeneo 4(60c)
Manispaa
kupitia sisi madiwani wake na watendaji, tuliliona hili kuwa ni hitaji
kubwa kwa wakazi wetu kwa ujumla, hasa makazi. Hivyo tulipendekeza ili
kuendana na kasi yakukua kwa uhitaji wa viwanja kunakotokana na kukua
kwa uchumi; ni vyema tukanunua vifaa bora kwaajili ya upimaji. Hivyo
manispaa yetu sasa ina vifaa vya kisasa vya upimaji ambavyo kwa Manispaa
zote Tanzania ni Manispaa mbili tu yenye navyo yaani Arusha na Iringa.
Vyenye uwezo wakupima viwanja 100 kwa siku. Viwanja 400 na zaidi
vilipimwa na kugawiwa eneo la ngelewala, 100 eneo la mafifi, na maeneo
mengine yanaendelea kupimwa.
Changamoto
tulio nayo ni kutokuwa na ardhi yetu wenyewe. Ardhi inayopimwa
tunaichukua kwa wananchi kwa kulipa fidia, kisha kupima kuwa uuzia au
kuwagawia watu tena. Fidia pia kwa kadri mji ulivyoendelea inakuwa kubwa
kidogo.
Utaratibu
wa ugawaji pia umeboreshwa. Kwamba kila fomu inayotolewa maanake ni
kiwanja. Sasa tulichogundua tena wanao kuja kuchukua fomu zile wengine
wanajihimu saa 10.00 usiku, sio wa hitaji wa viwanja wanakuwa tena
madalali.
Kwahiyo
kachukua fomu kwa 10,000/= anaiuza 50,000/= mpaka 200,000/=. Sasa hii
tena ni shida, cha msingi tunawaomba wananchi muwe mnasoma matangazo
yetu, au kusikiliza matangazo, maana hata kiwanja pia unaweza
ukalanguliwa.
Kuna
njia nyingine ambayo mnaweza kupiwa viwanja, kwa kuomba ofisi za ardhi
manispaa ziwapimie kwa kuchingia gharama kwa pamoja. Ila sharti
mtatakiwa mruhusu miundo mbinu yote kupita kwenye maeneo hayo, kama bara
bara nk.
MIPANGO MIJI-4(60b)
Sheria
za mipango miji zimeendelea kufuatiliwa, kuzuia ujenzi holela kati kati
ya mji. Natunawaomba wananchi waendelee kufuata sheria za mipango miji
ili kuruhusu kada nyingine kufanya kazi pia bila bughudha.
MKURABITA
Huu ni mpango wa Serikali ya CCM ambao ni mkakati wa Kurasimisha raslimali na Biashara Tanzania.
Kwa
lengo la kutambua rasmi au kisheria raslimali za wanyonge ambazo bado
ziko kwenye sekta isiyo rasmi, ili zitumike kuwawezesha washiriki kwenye
uchumi rasmi wa Taifa. Yaani kutambua nyumba ambazo zimejengwa katika
maeneo yanayoruhusiwa kisheria na taratibu, lakini hazina hati milki.
Ziweze
kukatiwa hati milki ili watu hawa wawe kutumia nyumba hizo kama
corallater au dhamana za kupatia mikopo katika taasisi mbali mbali za
fedha na kuboresha, kuinua au kuanzisha shughuli ya kumuinua mtu
kiuchumi na kisha kujitegemea.
Kwa
manispaa yetu ya Iringa chini ya usimamizi wa madiwani na kwa
kushirikiana na watendaji pia, kazi hii itaanzia Kata za Mwangata, kisha
hata Kitanzini tutanufaika na mpango huu wa MKURABITA.
MAJENGO/NYUMBA-4(60a)
Ujenzi
na aina ya nyumba zinazojengwa pia ni ishara ya maendeleo ya kiuchumi
ambayo pia huchochea uchumi kuendelea kukua. Nyumba nyingi zimeboreshwa
baada ya manispaa kutunga sheria ya kufungua vichochoro. Hii imetoa
fursa kwa nyumba nyingi kufungua milango ya maduka mengi ambayo yameinua
kipato kwa wenye nyumba na wapangaji pia. Vibali pia vilitolewa kwa
wenye nyumba kukarabati nyumba zao. Na wengine wamepata fursa ya kujenga
maghorofa yameongezeka, hali inayoashiria kukua kwa uchumi.
NISHATI-4(61)
Moja
ya matatizo makubwa yaliyikuwa yanavikumba viwanda vyetu pia, hadi
vikapelekea vingi vyake kuzaliza hasara ili kuwa ni upungufu wa nishati
ya umeme. Ikiwa ni pamoja na matatizo ya menejimenti. Hivyo naamini
mwaka huu mgao wa umeme umepungua sana, na kwa mikakati ya mbele pamoja
na upatikanaji wa gesi naamini itatusaidia kutekereza vyema sera ya
mapinduzi ya viwanda.
SURA YA TANO
UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
Lakini
ili wananchi ili waweze kumiliki uchumi lazima wawe na maarifa ya
kisasa. 5(76a) Ilani inasema kufufua kwa nguvu zote elimu yenye manufaa
ya watu wazima nchini kote ili masomo ya ujasiriamali,uwezeshaji,
urasmishaji wa biashara, kilimo, ufugaji na uvuvi yawezekutolewa kwa
wananchi wengi; Hatua za kutoa mafunzo ya ujasirimali lazima
zichukuliwe;
Ndugu wananchi ili watu waweze kujenga uchumi wa kujitegemea, hususani wananchi wa Kata ya miyomboni kitanzini.
Ambayo kwa kiasi kikubwa imesheheni wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
Wanahitaji kupata maarifa hasa ya Elimu ya ujasiriamali ili kufanya biashara zao kwa ufanisi mkubwa.
Ndugu
wananchi, mimi baada yakuliona hilo niliona umuhimu wakupata mafunzo
hayo ya ujasiriamali. Ambayo yalifanyika mara mbili katika ukumbi wa
warfare na Saba Saba CCM. Ambayo yalihusisha 1.utengenezaji wa bidhaa
mbali mbali za viwandani kama utengenezaji wa sabuni za miche, sabuni za
maji, dawa zakuoshea au kudekia, dawa za vyooni nk. 2.Usindikaji wa
vyakula mbali mbali. 3.Mafunzo ya ufugaji bora wa mifugo mbali mbali
kama kuku na utengenezaji wa chakula chake, Ng’ombe, mbuzi nk
USHIRIKA-5(76b)
Jumla
ya makundi 18 ya watu hamsini hadi sitini yawajasiriamali yalianzishwa
ambao jumla yao ni zaidi ya 1080. Na ofisi yangu ya Diwani iliwasaidia
kuandika katiba na kusajiliwa rasmi manispaa. Vikundi hivyo ni
Mshikamano, Saba saba no.1, 2,3; Nuru Group, Ebenezer Group, Tuwezeshe,
Amani, Nams Group, Juhudi Group nk Pia makundi ya vicoba ambapo katika
Soko la Mashine tatu pekee yake kuna vicoba vitatu. Idadi ya vikundi
vilivyoundwa katika Kata viko zaidi ya 20 na 15 vimesajiriwa tayari na 5
vinaendelea na mchakato wa usajiri. Hivyo jumla ya vikundi vyote 38.
Wajasiriamali
pia walielezwa fursa zilizopo zakukopa katika Taasisi za kifedha
zilizopo ndani ya Kata yetu na Nje kama mabenki kama NMB, na taasisi
nyingine kama FINCA, Pride na SACCOS na VICOBA.
Pia walielezwa na kufundishwa namna yakujiwekea pesa au kusave kama njia mbadala ya kupata mtaji.
AJIRA NA UWEZESHAJI WANANCHI-5(77)
UBORESHAJI WA MASOKO
Hii
pia ni njia mojawapo ya kujenga uchumi, kwani hutoa fursa kwa
wafanyabiashara kuendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa. Kutokana
na ongezeko kubwa la wafanyabiashara hasa katika kata hii, Manispaa kwa
kushirikiana na wadau wa soko kuu wameboresha soko kuu kwa kushirikiana
na wafanyabiashara. Lakini ili kupunguza msongamano masoko mawili
yameongezwa katika kata hii. Ambalo nimagari mabovu na mashine tatu ambalo
bado mpango wakuliboresha zaidi, hasa wakati wa masika unaendelea.
Kwani eneo hili linamilikiwa na wenzetu wa Bakwata pia.
Hata
hivyo mimi kama Diwani nimeweza kushirikiana na wana mashine tatu
kuhakikisha lile linalowezekana angalau kutunusuru mvua limefanyika kwa
kutoa trubai la kuezekea eneo la matunda.
FURSA ZA KIBIASHARA VIJANA-5(78)
Ndani
ya kata yangu vijana wengi wamenufaika na kuruhusiwa kwa biashara ya
pick-pick alimaarufu boda boda, ambazo zimetoa ajira kwa vijana asilimia
kubwa.
Pia
kuna fursa ya Toyo, mikokoteni ambayo kwa kiasi kikubwa inatupa
changamoto ya kuhakikisha bara bara zote zinatumika kwa matumizi
yaliyokusudia ya vyombo vya usafiri.
VIJANA
Mafunzo
ya ujasiriamali yalitolewa katika Chuo kikuu RUCO ambayo mimi mwenyewe
niliyatoa kwa vijana wa timu za mbili za mpira wa miguu kutoka katika
kila kata ambazo jumla zilkuwa timu 40 ukiongeza na za vijiji.
Pia
mitaji ya mabero ya mitumba nane ili tolewa kwa vijana wa timu za mpira
wa miguu mbili kutoka katika kata ya Miyomboni Kitanzini; ambazo ni
Maghorofani FC na mashine tatu FC. Pia gunia 10 za mahindi zilitolewa
kama mtaji kwa vijana wa mpira wa miguu Ipogolo United. Na sabuni za
kuogea zenye dhamani ya sh.700,000/= zilitolewa kwa timu ya mpira wa
miguu wanawake Ipogolo. Bero kumi za mitumba zilitolewa kwa vijana wa
Iringa Youth club; belo mbili zilitolewa kwa vijana wa kundi la maigizo
kihesa- Umati; Jumla ya fedha taslimu milioni mbili zilitolewa kwa
mabinti walioterekezwa na wazazi au watu waliowapa ujauzito; ambapo
niliwaanzishia kibubu program. Baiskeli zilitolewa kwa watoto wa mitaani
na mafunzo na mashine ya kujzia tyre upepo.nk
Wapiga debe, wasukuma mikokoteni, makuli, wauzaji wadogo wadogo;
Waliundiwa
uongozi na kupewa vitambulisho na unifomu ili kufanya kazi zao kwa
ufanisi. Lakini pia walipewa elimu ya kuepukana na tabia zinazowafanya
wadharaulike katika jamii kama;
· Wizi
· Ulevi uliokithiri
· Lugha za matusi
· Uchafu
Waheshimu
kazi yao na kuwa raia wema na pia washirikiane na polisi kwa ulinzi
shirikishi katika maeneo yao. Na mengine mengi yamefanya kwa vijana hata
yaliyo nje na Ilani ya uchaguzi. Kama kuwasaidia kuwalipia ada za chuo.
Kushirikianao katika sherehe zao kama mwaka mpya nk.
Kushiriki kuzindua kanda au CD zao katika matamasha mbali mbali. Kuichangia timu ya polisi na mageraza.
Kutelembea
wafungwa na kuwa misaada ya ya sabuni za kuogea 800 na limu za karatasi
kumi. Kuchangia mikutano ya vijana wa CCM, Kuwasaidia hata wale vijana
ambao sio wa upande wetu. Kuchangia uanzishaji wa vikundi wa vya
kijasiriamali kama Ipogolo. Kushiriki katika shughuli za kijamii; kama
misiba, harusi, sherehe za vyuo vikuu, makanisa, misikiti nk.
MIUNDO MBINU
MAWASILIANO na USAFIRISHAJI/UCHUKUZI
Ndugu
wananchi katika kukuza uchumi, mawasiliano ni kitu cha muhimu, ambayo
huwezeza mzunguko wa biashara au huduma kuwa rahisi. 2.(d). Mawasiliano
ya simu za mkononi na hata za meza ndani ya kata yetu hakuna shida. Watu
wanaagiza mizigo kwa simu wanatuma pesa kwa simu. Hivyo imesababisha
kurahisiha ufanyaji wa biashara nakuongeza tija na maendeleo. Hata Kata
yetu haitakuwa na matatizo yo yote kuhama kutoka analogy kwenda
digitaly.
BARA BARA
Bara bara zimeimarishwa katika kata yetu na zinapitika kwa misimu yote kwaasili mia 99% kama sio 100%.
Mapungufu
madogo yalipotokea mwaka jana wakati wa mvua kubwa basi, marekebisho
yalifanyika hasa kwa bara bara ya mtaa wa mlimani. Bado tunachangamoto
kwa Bara bara kubwa karibu na eneo la sigara ambalo mara nying mvua
zikinyesha maji hufulika kwa kuwa karavati la eneo lile limetitia hivyo
kushindwa kupitisha maji kwa wingi. Swala hili limefikishwa kwa mamlaka
husika yaani Tanroads na wameahidi kulishughulikia wakati wa mchakato wa
kutengeneza bara bara ya Iringa mpaka Dodoma.
Ununuzi wa Greda
Kwakuona
pia mara nyingi bara bara zetu zinaharibika hasa wakati wa mvua kubwa
kama mwaka jana. Nausumbufu unakuwa mkubwa, pia kwakuwa tulikuwa
tunataka kila sehemu tunapopima viwanja angalau tutengeneze njia za
mitaa inayoonyesha jinsi viwanja vilivyogawika.
Basi,
tulipendekeza madiwani ufanyike uchakato wakutafuta greda. Ambao
ulianza kwa kurasmisha mali zetu za manispaa hasa majengo ambayo
hayakuwa na hati, ili tupate dhamana yakutosha kuwekezea ili tuweze
kukopesheka. Mchakato ukakamilika hatimaye, tukakopeshwa fedha na benki
ya CRDB ambayo imetuwezesha kununua Greda.
SURA YA SITA
HUDUMA ZA JAMII- ELIMU
MSINGI – 6(85
Ndugu wananchi; ndani ya Kata yetu tuna shule ya sekondari Miyomboni na sule ya msingi ni Azimio.
Watoto
wote wenye umri wa kujiunga na shule ya msingi yaani miaka saba
wamepata nafasi ya kujiunga na shule ya msingi kwa…….asilimia
Ili
kubaini matatizo yanayowapata watoto wa shule za msingi nilifanya nao
mkutano. Walitoa kero zao na ziliwasilishwa kwa Mkuu wa Shule; ikiwa ni
pamoja na kuomba walimu wasiuze, vitu darasani. Kwani huwa
vinawapunguzia umakini katika kusoma wanapofundishwa, kwa kufikiri kitu
kinachouzwa na kupopeshwa. Lakini pia huwasababishia kutoroka shule
wakikopeshwa wakakosa hela ya kulipa; huogopa kwenda shule.
Watoto
pia waliomba wazazi wao kuwa karibu nao nakupata muda wa kuwasikiliza
wanapokuwa na shida. Hasa kuwapa chai yenye kitafunwa asubuhi. Akina
baba pia wasiwaonee akina mama na akina shangazi.
Kero
yao nyingine kubwa ni kutokuthaminiwa hasa kwa kutowatengea au
kuendeleza maeneo ya michezo. Hivyo waliomba mipira na jezi. Timu mbili
za watoto walipewa mipira na jezi, ambazo ni Kitanzini United Stars na
Mshindo wanderous.
WALIMU
Pia walitoa mapendekezo na malalamiko yao huku wakiomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa wazazi; ili kujenga malezi bora.
Wakitoa
mfano wakukosa ushirikiano walisema ni pale walipobaini kuwa mtoto
mmoja aliyekuwa akisumbua sana na mtoro wad rasa la sita alipowajibu
amechelewa kwenda shule alikuwa kuwekwa vipandikizi vya kuzuia mimba. Na
hii ilionyesha wazi kuwa mlezi alikuwa anajua.
Pia
walitoa malalamiko ya baadhi ya changamoto wanazokutana nazo kama wizi
uliokithiri kwa maeneo ya shule, ukarabati wa shule kuwa muhimu, pia
nilipata fursa ya kuchangia mahitaji ya shule hiyo. Pia tuliwaomba
polisi kusaidia ulizi wa maeneo hayo. Usimamizi wa karibu zaidi upo
chini ya kata ya mshindo.
SEKONDARI
Kuwa
sekondari ya Kata, kuendelea kusimamia ufaulu wa kuhakikisha zaidi ya
asilimia hamsini ya watoto au zaidia wanafaulu na kujiunga na kidato cha
kwanza ifikapo mwaka 2015. Kiwango cha ufaulu kwa watoto wetu Miyomboni
kimekuwa kikiongezeka kwa……….
UJENZI,
Ilani inatakakuendelea kuboresha shule kwa ujenzi wa maabara, madarasa, vyoo, nyumba za walimu, nakununuavifaa vya shule.
Sisi tumeendelea kujenga maadhi ya majengo katika shule yetu ya Miyomboni kama;
· Madarasa mawili kwa mwaka jana yanatumika
· Vyoo matundu 14 kupitia mradi wa TASAF na uwekaji wa maji katika vyoo.
· Tumetengeneza madawati 180 kupitia TASAF
· Tumetengeneza pia vifaa vya ofisini kama meza 4, makabati ya walimu 4, mbao za matangazo 2 na viti.
· Tumeingiza umeme kupitia mradi wa TASAF
· Tunaendelea na ujenzi wa maabara kupitia mapato yetu ya manispaa.
WALIMU
Kutokana
na mazingira ya Kata yetu tunashukuru tumeendelea kupata walimu, na
hasa walimu wa field kutoka katika vyuo vikuu vinavyotuzunguka na vya
nje.
Hii
imesaidia kupunguza tatizo la upungufu wa walimu. Hata hivyo Serikali
inaendelea kudahiri walimu wengi zaidi ambao baada ya miaka 4 ijayo
watashindwa tena kwa kwenda. Ushauri vijana wetu wanao fikiria kujiunga
na fani hii wafikirie pia kupambana na changamoto hiyo. Au walimu wenye
degrii pia wataendelea kufundisha mpaka chini.
MAFUNZO YA UFUNDI
Baadhi
ya vijana wetu waliohitimu kidato cha nne katika Shule yetu
wamefanikiwa kujiunga na Elimu ya ufundi katika vyuo mbali mbali vya
VETA, hata hapa Iringa.
SEKTA YA AFYA-86
Ilani inataka kuwepo na miundo mbinu ya kutolea huduma katika Afya na ustawi wa jamii hasa katika ngazi ya vijiji na Kata.
Upimaji Clinic;
Kata
yetu inavituo vinavyotoa huduma hizi kama dispensary za private; lakini
tuna kituo cha kutolea huduma za Clinic karibu na ofisi ya mtendaji wa
Kata. Ambacho kati ya januari mwaka 2012 na januari 2013 kimetoa huduma
za upimaji kwa watoto wa Clinic chini ya miaka mitano watoto 7113.
Upimaji huu umezidi zaidi ya lengo la Kata lakuwapima watoto 4200 kwa mwaka. Na upimaji huo bado unaendelea.
Utoaji wa Chanjo;
Januari
hadi disemba 2012 zilitolewa chanjo kwa watoto wapatao 2448. Utoaji huu
pia upo kwa asilimia kubwa, zaidi ya lengo………la watoto katika Kata kwa
mwaka.
Kuzuia Malaria
Serikali
iligawa neti kwa kila kaya, na kata yetu pia tuligawiwa ikiwa pia ni
pamoja na wajawazito waliopata uzauzito walipewa neti kwa hati punguzo
kwa kulipia neti moja shilingi 500.
Lakini
Elimu mbali mbali zimeendelea kutolewa kuhusiana na umuhimu wa
kukabiriana na Malaria. Hasa ukizingatia huu ni ugonjwa unaoua zaidi ya
magonjwa mengine katika Nchi yetu.
Changamoto
imekuwepo, baada ya wanachi wengine kuamua kutumia neti kwa matumizi
ambayo haya kukusudiwa. Wananchi unaombwa kuunga mkono juhudi za
serikali katika kulinda afya zenu.
Kutunza mazingira
Ni
mkakati mojawapo wa kuzuia malaria upo kwenye Ilani. Ndiyo maana
watendaji wamitaa wakishirikiana na idara ya afya wamesimamia kwa zoezi
la usafi, hasa kuzuia maji yanayotiririka ili kuondoa madimbwi na nyasi
ambayo ni mazalia ya mbu. Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya
usafi katika Kata yetu.
Bado kuna tatizo la watu kuwa wakaidi na kutotaka kufuata sheria za afya na utunzaji wa mazingira.
Lakini
hata hivyotuwapongeze wananchi kwa juhudi kubwa zakuendelea kufanya
usafi. Ambayo kwa mika yote ilitufanya manispaa yetu kuwa ya pili Kitafa
kwa minispaa kiusafi, isipokuwa mwaka jana ambapo tulishika nafasi ya
nne.
Hii
ilitokana pia na kuwa na tatizo kubwa la Skip Buskets au madapo; ambayo
kwa kiasi kikubwa yalichakaa kutokana na wananchi kuyaunguza kwa
kuwasha moto, au kumwaga moto ndani yake. Hivyo yamekuwa hayatoshelezi
kwa hiyo hii imepelekea watu kutupa uchafu ovyo.
Lakini pia ukosefu wa magari ya uhakika ya uzoaji wa taka taka. Kutokana na yale yaliyokuwepo kuchoka.
Mkakati
uliopo ili kutatua swala hili; wa haraka kwanza ofisi ya manispaa afya
wanahitaji vikundi vyakusimamia usafi, kutoka katika maeneo yetu. Mtu
akionekana anatupa uchafu ovyo atakamatwa na kupigwa faini ambayo
watagawana kwa percent.
Mkakati
namba mbili ni uliwa maombi ambao tumetuma, madiwani na tumeahidiawa
kusaidiwa na world Benki kwenye swala hili pia la Magari ya kubeba taka
na madampo 100.
NB: Kwenye
miradi hii ya world benki tuache siasa za uongo. Wale wenyewe wanataka
wananchi kwa ujumla wetu tuelewe kwamba world bank ndiyo wanao saidia na
ninyi mnaelewa mnasasidiwa nini na wao? Ndiyo moja ya vigezo ili
waendelee kutusaidia kwa muda mpaka 2017. Pia tuonyeshe mabadiliko kama
jamii, kama tulikuwa tunachoma skip busket-madampo safari hii tuache.
MAJI-6(87a)
Ilani
inasema Kuongeza huduma za upatikanaji wa maji kwa silimia 75% vijijini
na mijini 95% ifikapo mwaka 2015. Kwa manispaa yetu ya iringa
apatikanaji wa maji ni asilimia……….
Mtandao
wa maji taka na safi imeimarishwa sana katika Kata yetu. Wananchi
mmeshuhudia jinsi ambavyo maji yamekuwa yakiendelea kuunganishwa ndani
ya Kata yetu, ambayo chanzo chake Mh.Raisi wa Jamhuri ya Muungano
Tanzania alikuja kufungua rasmi baada ya kukamilika kwake. Changamoto
tulio nayo pia ni presha ya maji kubwa hivyo kupasua baadhi ya mabomba
hasa yanayoingia majumbani. Pia wizi wa maji kwa kunyonga mita, hali
iliyowapelekea IRUWASA kuhamisha mita kutoka ndani kwa watu au sehemu
zilikojificha na kuweka nje au sehemu nyeupe ili zisihujumiwe.
Mtandao
wa maji machafu pia umepita katika kata yetu. Hivyo wananchi unaombwa
kuhakikisha hamtiririshi maji machafu bali muuombe kujiunga kwenye
mtandao wa maji taka.
Pia
ilani inatutaka kuimarisha utunzaji wa vyanzo vya maji. Hivyo tunaomba
wananchi ujenzi holela kwenye mabonde na vilima usifanyike, ili
kuendelea kuwa na uhakika wa hali ya hewa nzuri, na upatikanaji wa maji.
Maji haya vyanzo vyake vyote inategemea vyanzo vya maji. Sasa hata kama
tuna mtandao mzuri wa mabomba kama maji huko chini hakuna bado
hatutakuwa na maji.
SURA YA SABA
MAZINGATIO MAALUM YA ILANI KUHUSU ZANZIBAR
Yanawahusu wa Zanzibari.
SURA YA NANE
Maeneo mengine muhimu;
MUUNGANO
Sisi kwa Ilani hii tunaendele kuimarisha muungano ambao utafikisha takribani miaka 49 ifikapo tarehe 26 April 2013.
Kwa
nia yakujenga amani, mshikamano,umoja na kushirikiana kiuchumi ili
kuimarisha uchumi wa pande mbili ambapo wazanzibari wanafikia 1dadi ya
takribani watu 1,300,000 na kidogo.
Mpaka
katiba itakaposema vinginevyo, kwa ilani hii muungano sawa sawa na
unahitajika kuimarishwa na kurekebisha kasoro ndogo ndogo zinazoleta
kwanini?
UTAWALA BORA
Umeendelea
kuimarishwa kwa kutoa haki kwa wanaostahili ikiwa ni pamoja na kutoa
vyeti vya ufanyakazi bora kwa watumishi wa wetu ndani ya manispaa na
zawadi mbali mbali waliofanya vizuri. Lakini adhabu stahili zimetolewa
kwa waliofanya ndivyo sivyo.
Mwenendo
wa madiwani pia umethibitiwa kupitia kamati za maadili, ingawa wengine
wanaona kama kufanya fujo na kutoanyesha nidhamu kwa kufuata taratibu,
kutoa lugha za matusi dhidi ya wenzao, kusema uongo nk. kuwa ni sifa ya
kujipatia umaarufu kisiasa.
Hapa hukumu itatoka kwa wananchi na kwa Mungu aliyeridhia wote wawe madarakani.
Sekta ya Sheria-187
Manispaa inakitengo cha Sheria ambacho kinasimamia sheria zote za manispaa.
Ikiwa ni pamoja na wagambo wanao zuia matumizi mabaya ya miundo mbinu, tofauti na makubaliano.
Kutokana
na mazingira ya kata yetu, kuwa ndiyo kitovu cha mji, ofisi za magereza
zipo hapa na magereza yenyewe, Hospitali kubwa tunapakana, kituo
kikubwa cha polisi, masoko yote, maduka makubwa mengi, stendi zote kubwa
kwa mabasi makubwa na hiace, boda boda, Toyo, ofisi za fire nk.
Inatulazimu
kuhakiksha bara bara zote zinakuwa wazi ili kuruhusu sekta nyingine pia
kufanya kazi bila usumbufu, kama fire, magereza, polisi hospitali,
wasafirishaji nk.
Tunaomba
wananchi muondoke bara barani mnakofanyia biashara. Kuna nafasi za
masoko mashine tatu, magari mabovu, ngome, Kitwiru nk.
Kuhusiana
na kufungua Bara bara ya magereza kwenda Hospitali, mchakato
unaendelea, ili kuona salama ya wagonjwa itakuwaje na kelele za magari?
Lakini pia kuona gereza itakuwaje?
Tunalishughulikia
kwa kuwashirikisha wadau wote. Lakini kuona pia kama tunaweza kutumia
utaratibu mwingine wakutumia bara bara ya juu kwa upande wa mkuu wa
wilaya.
Demokrasia na maendeleo ya Umma;
Ilani inataka demokrasia kukua nadhani. mnaona uhuru wa wananchi, kujieleza ingawa uhuru bila mipaka ni vurugu.
Wenye uelewa hafifu hutumia vibaya kwa kutafuta umaarufu wa kijinga.
Demokrasia
imetumika katika kujipangia maendeleo ambapo watu kuanzia ngazi ya
mitaa wameshiriki kupitia wenyeviti wa mitaa wanao wachagua, kisha
kuunda baraza la maendeleo la Kata kwa kutumia wneyevit wa mitaa, diwani
wa kata ambaye ni muwakilishi wa wananchi.
Hivyo ni muhimu kuhudhuria mikutano ya Mitaa ili kuibua au kushiriki katika mipango ya maendeleo.
Mfano kumekuwa na mahudhurio hafifu sana ya vikao au mikutano ya mitaa ya maweni, Jamaat na Miyomboni.
Lakini
ukikutana nao mitaa au bara barani wanakupa kero ,ooh mh.miziki mikubwa
tunashindwa kulala, wauza samaki wabichi wanatunukia nk.
Hizi
kero Serikali ya CCM imewawekea utartibu mzuri mkutane kwenye mtaa
mfanye mkutano, mkiuhusisha na mhusika, na kumwambia kero yenu, akiwepo
mtendaji wa mtaa na Mwenyekiti wa mtaa hao ni Serikali kamili na
wananguvu Kisheria.
Baadaye
katika mtaa wenu mnaweka maazimio yasipotekelezwa mnapeleka mbele,
ngazi ya Kata kisha yatafika manispaa, na hivyo kushughulikiwa kirahisi
na mtapata mrejesho hivyo hivyo.
Kushiriki
kwenye miradi ya TASAF kwa kutumia kamati za mitaa kutekeleza miradi au
kutumia mkutano wa mtaa au vikao kuibua mradi wa mtaa wenu.
Mfano vyoo vili 14 matundu ya Miyomboni Sekondari uliibuliwa na mtaa wa Stendi kuu. Leo watoto wa shule nzima wanatumia vyoo.
Sasa
mtaa wa stendi wangekuwa hawafanyi vikao ingekuwaje? Kwanini
imerudishwa mtaani kwa kuwa kila mtaa unamatatizo yake, kutokana na eneo
na shughuli zinazofanywa na mitaa husika.
Miyomboni
ni wafanyabiashara wengi, kwa hiyo mna kero za ushuru wa huduma,
usumbufu wa fire, nk. Mkikaa kikao cha mtaa mnatuletea, mapema kwa
uangalifu, na kwa utartibu stahiki. Tutaangalia mgogolo unaanzia wapi
kisha tuta tatua.
MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
Ilani inatoa maelekezo namna yakupambana na rushwa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha TAKUKURU.
Lakini
swala la Rushwa lina mhusu kila mmoja wetu. Jiangalie wewe umewahi
kupokea au kutoa Rushwa iwe ya kitu, hali, ngono au fedha? Ukiona
umewahi unatakiwa wewe kuwa wa kwanza kuacha kama ni kupokea au kutoa
Rushwa.
Serikali inajitahidi kutoa elimu kuhusu Rushwa na kwa kuwa watoa Rushwa na Wapokea Rushwa ni wana jamii au watu.
Basi
wakiingia kwenye siasa wanakuja nazo; wakiingia kwenye biashara wanayo,
wakiingia makazini wanazo, wakiinga hata kwa uchache hata kwenye
taasisi za kidini wanazo.
Hili ni tatizo ambalo limekuwa kama utamaduni ambao unahitaji mchango wa kila mwanajamii, kupambana nalo.
Lakini inakuwa afadhari watu wanafichama kwa kuogopa TAKUKURU kidogo.
Ulinzi na Usalama;
Polisi wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuzuia ujambazi katika Kata yetu hasa ule mkubwa.
Lakini
bado kunatatizo kubwa la vibaka na wezi wadogo wadogo. Ila uvutaji wa
bangi na matumizi ya madawa ya kulevya hasa kwa vijana imekuwa
nitishio.
Ofisi
yangu kwa kushirikiana na uongozi wa Iringa Youth club uliendelea kutoa
mafunzo ya namna yakujiajili na kuachana na madawa ya kulevya na tabia
hatarishi zisizokubalika katika jamii.
Hilo tunawashukuru Jeshi la polisi.
Kwa
shughuli za Kata yangu kama isingekuwa doria za uhakika kila siku
ubomoaji wa maduka na uvamizi ungekuwa hatari, hasa kwasababu vyakuiba
na vyenye faida vipo.
Kata yangu imeshirikiana na polisi katika maswala ya ulinzi shirikishi kwa kuwa na polisi kata.
Lakini kuanziasha mchakato wa sungunsungu. Kata yetu pia inamlezi wa kipolisi.
Pia
vijana wameendelea kupata fursa ya kujiunga na JKT na JKU. Ili
kuwawezesha kujiunga na Jeshi la polisi, ili kulinda Nchi pamoja na
makampuni mbali mbali ya Ulinzi, nakuwajengea uzalendo zaidi.
Kwa
wale walio msikia mkuu wa wilaya juzi redioni waliwaalika pia vijana
wengine kutoka katika wilaya yetu, kupeleka maombi ya kujiunga JKT. Mimi
nafikiri wale mabaunsa wanao tulinda na wakati mwingine wanatutisha
tisha wakajiunge ili wawe rsmi zaidi.
Hifandhi ya Mazingira;
Manispaa
inakitengo kinachoshughulikia hifadhi ya mazingira ambayo huangalia
misitu yetu, na pia huzalisha mbegu za miti ambazo huwa zinagawiwa kwa
mashule ili kupanda; lakini hata wananchi wanpata fursa ya kununua na
kupanda.
Pia kuna sheria inayomtaka kila mwenye nyumba kupanda miti mitano katika eneo lake. Hivyo ni muhimu tukaitekereza.
Pia kuna vikundi vya utunzaji wa mazingira vya mitaa. Nadhani katika Kata yetu mtaa wa Mlimani wanatunza miti pia.
Mnaweza
kufaidi zaidi misitu hiyo kwa kufunga nyuki, kwa mazinga mmoja bora
unaweza ukakupa asali lita 20 ambayo ni sh.150,000 – mpaka 200,000/=.
Na
kwa kukiboresha kitengo hiki ilikusaidia kutoka kata miti ovyo Serikali
kupitia wizara ya maliasili imewekeza sana kwenye ufugaji wa nyuki, na
mabwana nyuki wapo, tuwatumie.
Kujenga uwezo wa kukabili majanga;
Kwa
kuanzisha kitengo cha maafa, ambacho hushughulika inapotokea maafa.
Bahati nzuri mwaka jana hatukuwa na maafa katika Kata yetu.
Vyombo vya Habari;
Vyombo vya Habari vinajukumu la kuhabarisha,kuburudisha na kuelimisha.
Ilani
inaitaka Serikali iendelee kulinda uhuru wa vyombo vya habari, lakini
itaanzisha chombo ambacho kitahusika kudhibiti ukiukwaji wa vyombo vya
habari na kusimamia maadili ya waandishi wa habari.
Nadhani
kimeshaanzashwa niliona kinazinduliwa kwanye TV. Pia ilani
inazihamsisha harimashauri kuanzisha vituo vya utangazaji, pamoja
Television,ili kuwapa wananchi habari.
Sisi
manispaa ya Iringa tumetekeleza hili kwa kuanzisha kituo cha IMTV,
nabado tumeednelea kukiboresha kwa kukitengea bajeti ilikifanye vizuri
zaidi.
Kujenga
mahusiano mazuri na waandishi wa habari. Mimi binafsi nina mahusiano
nao mazuri. Tunashirikaina wakati wa Raha na shida, tukikanyagana ni
kawaida kwa watu wanaotembea pamoja.
Nimeshiriki
kwa ukamilifu mkubwa katika kusherekea siku ya waandishi wa habari
duniani; Nimetoa maoni yanga na mchango wangu wa mawazo na mali katika
kuimarisha tasnia hii ya habari. Hata wao huwa wana ni miss nikiwa sipo
wakinialika, lazima wanitafute hata kwa teknolojia ya simu ili
tushirikiane. Hafu wananikubali kama mtu bora. Hivi wamesema haiwezekani
mpaka nije niwafundishe ujasiriamali. Niliwaambia nipo tayari
mtanisikia mkiwa tayari.
Lakini
mimi pia ni mteja wa vyombo wa habari kwa kutoa matangazo kwa kulipa;
na kutoa mafunzo kwa kulipia pia. Kwahiyo cha msingi hapa tuendeleze
maahusiano yetu kibiashara na kijamii, tusiingize itikadi zetu kwenye
taaluma na biashara au huduma na kazi.
Mambo ya Nje;
Unasafiri
kwenda Nchi nyingine ni kwasababu yautekelezaji uliofanywa na Serikali
ya CCM kupitia Ilani hii kama wasinge wafanya kitu hata wewe usiruhusiwa
kuingia huko Nchi za watu.
Watoto
wetu, ndugu jamaa na marafikia wapo Nje kwa sababu,Ilani hii imejenga
utaratibu wakuwawezesha watanzania kukubalika Nchi nyingine.
Angalia Nchi zilizokosa utaratibu watu wanapata shida kuingia Nchi nyingine wanasafiri kwenye matanki ya mafuta wanaishia kufa.
Pia nikutokana na amani, umoja, utulivu na mshikamano wa Kitaifa, huu unatujengea heshima hata kwa Nchi nyingine.
Utamaduni na Michezo;
CCM kinaamini kwamba vijana wa Tanzania wana vipaji vya michezo mbali mbali kama walivyonavyo wenzao wa Mataifa mingine duniani
Kwa kulitambua hili manispaa yetu imeendelea kuzuia ujengaji katika maeneo yaliyotengwa kwaajili ya michezo, na open space.
Pia katika michora ya mipango miji maeneo ya ngerewala kwa ushauri wa madiwani tumeingiza Satdium
Pia tumetenga bajeti angalau kwa kila Kata kupat mipira mitano, ikuwasaidia vijana.
Ndugu
wananchi mimi binafsi katika swala la michezo kama diwani. Nilianzisha
mashindano ya mpira wa miguu yanaoitwa Jesca Cup ambayo yalifanyika kwa
ngazi ya Kata; ambapo kila Kata ilitoa timu mbili, wakaunda kanda za
kata tano tano kwa ngazi ya kata, ambapo Kata zilicheza timu kumi.
Kila
timu zilizo shiriki timu 34 na kuongeza za vijiji sita jumla 40 wenye
wachezaji 25 na viongozi wa timu, walipata mafunzo ya ujasiriamali RUCO;
kama ilivyoelezwa huko juu, lakini pia wote walipata mpira mmoja
mmoja.
Wasimamizi
wao waliokuwa sta maana tulipata kanda sita walijitolea na kuwezeshwa
vocha kido kama 50,000/= ili wasimamie michezo hiyo.
Baadaye tuliingia ngazi ya manispaa ambapo tulipata timu kumi bora kutoka kanda zota ambaye ni mshindi wa kwanza na wa pili.
Ambao walipe zawadi ya jezi kwa mshindi wa kwanza na mipira 2 kwa mshindi wapili.
Katika
fainali mshindi wa kwanza alipewa jezi, kombe na mipira miwili, wapili
jezi na ngao na mpira na watatu jezi na mipiara miwili.
Timu
yenye nidhamu ilipewa jezi, kipa bora alipewa mpira,na marefa
wacheshaji walipewa jumla 200,000/=. Msimamizi pia alipewa jezi kwaajili
ya timu yake.
Katika kata ya kitanzini timu yetu ya mashine tatu nilikuwa nayo karibu ikiwa nipamoja na kuwapongeza pale walipofanya vizuri.
Lakini
kuwaanzishia pia mradi wa kuichumi, kwa kuwapa bero 4 za mtumba, Na hii
ndiyotimu inayoongoza kwa makombe mengi katika manispaa hii ikiwa ni
pamoja na kombe la RPC kamwanda, Jesca Cup nk.
Maghorofani pia walifanya vizuri hii ni ya kitanzini wakachukua ubingwa wa kwanza kwenye ligi ya wilaya.
Tuna
timu nyingine ya uhuru FC washona viatu, Timu ya stendi kuu walipata
jezi, madereva tax stendi pia walipata jezi na timu ya madrasa kitanzini
pia tuliwapa jezi.
Pamoja na timu nyingine zaidi ya kumi kutoka maeneo mengine kama Mlandege na kata zingine.
Mpira wa wanawake tulishirikiana na IDYC katika kupromote mpira wa miguu kwa wanawake.
Ambapo
mimi nikiwa kama mgeni rasmi, timu za watoto wa kike zilishiriki katika
mashindano hayo katika viwanja vya Ulandege. Ambapo pia alialikwa
kampteni wa timu ya Taifa Twiga stars Pulkaria kuja kuwa tia moyo.
KUYAENDELEZA MAKUNDI MBALI MBALI
Watoto;
Watoto
nikama nilivyeelezea kuwa nimefanya nao mikutano, na kusaidia
kuwafundisha maadili na kuwasadia kuwa semea mahali husika kuhusu
matatizo yao.
Nimepet fursa ya kuwatembelea watoto wa vituo vya yatima, Kitwiru, Tosamaganga, Ilala Nvinureny nk.
Wanawake
· Pia nimefanya nao mikutano na walieleza changamoto zao ambazo zilipelekea kuwatafutia fursa ya kupata mafaunzo ya ujasiriamali.
· Nimewasaidia katika kuanzisha vikundi na kuwasadia kuandika katiba na kuvisajiri.
· Ni
metembelea vikundi mbali mbali vya akina mama mfano mlandege-NAMS
watengenezaji wa Batiki na kuwatafutia masoko, mashine tatu, orophare
kitanzani, Wajane TRM, vikundi vya makanisani mbali mbali na kuto elimu
ya ujasirimali nk.
Wazee;
· Nilifanya, mkutano na wazee wote. Mawazo yao yalisaidi akuboresha shule zetu.
· Lakini pia nilipata fursa ya kutembea kituo cha wazee kitanzini mara kwa mara.
· Pia niliwatembelea wazee wa majumbani wakati wa sikuku ya Idd ilikuwatika sherehe njema.
Watu wenye ulemavu;
· Nilipata fursa yakuwatembelea wenye ulemavu wa macho, au wasiona na kuwasikiliza changamoto zao. Niliwatia moyo.
· Lakini pia niliweza kuwasidia ili waweze kwenda kwenye mkutano wa wasiona kitaifa, huko Mtwara. Au maarufu kama siku ya fimbo.
· Watoto
wa mitaani kuna mmoja na msomesha Kreeluu Sekondari, Wengine nimewapa
Baiskeli waliomba kwaajili ya kufanyia vibaru vya kusomba mchanga.
Nilijitahidi kuwasaidia misaada mbali mbali. Ikiwa na kuwapa ushauri
nasaha.
UKIMWI
UKIMWI bado limeendelea kuwa ni tatizo kubwa katika mji wetu hata Kata yetu ya Kitanzi.
Juhudi
mbali mbali zimeendelea kufanyika kuendelea kutoa Elimu kupitia
Mikutano, vyombo vya habari na matangazo mbali mbali ya mabango nk.
Ili kuzuia maambukizi mapya na kuzuia kuongezka kwa UKIMWI kwa ujumla.
Pia kuendelea kugawa dawa kwaajili ya kupunguza makali ya UKIMWI kama ARV’s.
Pamoja
na kutoa Elimu ya magonjwa nyemerezi na magonjwa ya ngono. Katika kituo
chetu cha Angaza kimeendelea kutoa huduma ya Upimaji na Zaidi ya 12,000
wamepimwa kati ya mwaka 2010 -2012.
SURA YA TISA
Inawahusu
wenye Ilani hii ambao ni CCM. Sasa leo nipo kama Diwani haya
tutaelezana ndani ya Chama. Hasa hasa kuisimamia kivitendo utekelezaji
wa Ilani hii.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA. NA KARIBISHA MASWALI
TAARIFA YA UTEKELEZAJI KATA
KITANZINI
ILANI 2010-2012
Imeandaliwa:
DIWANI; JESCA J.MSAMBATAVANGU
P.O.BOX 2464, IRINGA.
TANZANIA. MOB:0754-301349
Post a Comment