Timu
ya Azam FC imewasili salama jijini Nairobi nchini Kenya jana usiku tayari kwa
kuanza michezo yake wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili
ya ligi kuu ya Tanzania mzunguko wa pili pamoja na mashindano ya Kombe la
Shirikisho Afrika.
Akizungumzia program nzima
ya maandalizi kocha wa Azam FC, Stewart Hall amesema timu itacheza mechi tatu za
kirafiki na kufanya mzoezi ya siku mbili katika viwanja vya Nyayo na
City.
Alisema wachezaji wote
wamefika salama, timu itaacheza mchezo wake wa kwanza kesho ‘Jumamosi’ saa 3:30
(15:30hrs) dhidi ya A.F.C Leopard, kwenye Uwanja wa Nyayo.
Azam FC leo ‘Ijumaa’ jioni
itafanya mazoezi yake ya kwanza katika Uwanja wa Nyayo uliopo katikati ya jijini
la Nairobi.
“Tutacheza michezo mitatu,
michezo yetu itahusisha timu zenye viwango vizuri katika ligi ya Kenya ambazo ni
A.F.C Leopard, Sofapaka na K.C.B, mechi hizo zitasaidia kuimarisha timu yangu”
alisema Stewart.
Kocha Stewart alisema
watafanya mazoezi na kucheza mechi katika viwanja aina mbili vyenye nyasi za
kawaida na zenye nyasi bandia kwa kuwa katika michezo ya ligi viwanja hivyo
vinaendana na mazingira ya Tanzania.
Azam FC iliyoko nchini hapa
bila ya washambuliaji wake John Bocco na Tchetche Kipre na mchezaji Waziri Salum
wanaosumbuliwa na majeruhi, siku ya Jumapili itacheza mechi yake ya pili ya
kirafiki dhidi ya SOFAPAKA kwenye uwanja huo huo.
Baada ya mchezo huo kikosi
hicho kitapumzika siku ya Jumatatu Jan 21, 2013 ambapo watatumia siku hiyo
kufanya mazoezi katika Uwanja wa City wenye nyasi bandia.
Azam FC itamaliza safari
yake ya maandalizi na mechi za kirafiki siku ya Jumanne Jan 22 ambapo watacheza
dhidi ya K.C.B kwenye Uwanja wa City mchezo ambao utakamilisha safari hiyo ya
siku saba.
Wachezaji walioko jijini ni
Mwadini Ally, Aishi Manula, Jackson Wandwi, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David
Mwantika, Luckson Kakolaki, Jockins Atudo, Michael Bolou, Humphrey Mieno, Khamis
Mcha, Gaudence Mwaikimba, Uhuru Selemani, Brain Umony, Malika Ndeule, Omary
Mtaki, Abdi Kassim ‘Babi’, Abdalah Seif, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo na Salum
Abubakar ‘Sure Boy’.
Post a Comment