Shujaa
Mwaikimba baada ya kufunga bao la ushindi usiku huu |
Na Mahmoud
Zubeiry, Zanzibar
AZAM FC
wamefanikiwa kutetea Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan,
Zanzibar baada ya kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao
2-1.
Kwa ushindi
huo, Azam wamezawadiwa Sh. Milioni 10, wakati washindi wa pili Tusker wamepata
Sh. Milioni 5.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Ramadhan Rajab Ibada ‘Kibo’ aliyesaidiwa na
Mwanahija Makame Mfumo na Mgaza Kindundi, hadi mapumziko hakuna timu
iliyofanikiwa kupata bao.
Azam ndio
walioshambulia zaidi katika kipindi hicho, lakini hawakuwa na bahati ya kufunga
bao japo moja. Gaudence Mwaikimba alipewa pasi nzuri na Brian Umony dakika ya
44, lakini shuti lake kali lilidakwa na kipa Samuel
Odhiambo.
Kipindi cha
pili, Tusker walirudi na moto mkali na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo
langoni mwa Azam.
Hiyo
iliwasaidia mabingwa hao wa Kenya kupata bao dakika ya 60, lililofungwa na Jesse
Were aliyeunganisha kwa shuti kali la kimo cha mbuzi pasi ya Robert
Omunok.
Hata hivyo,
bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC walisawazisha dakika ya 72 lililofungwa
kwa mkwaju wa penalti na beki Mkenya, Joackins Atudo baada ya beki wa Tusker,
Luke Ochieng kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Katika
dakika mbili za nyongeza baada ya kutimu kwa dakika 90 za mchezo huo,
alijitokeza binti mwenye umri kati ya 14 na 16 na kukatiza uwanjani akitokea
jukwaa la Urusi
Refa
alijaribu kumsimamisha, lakini aliendelea kukatiza Uwanja hadi nje ambako
alipokewa na askari Polisi na kutolewa nje kabisa ya Uwanja. Mtangazaji wa
Uwanja wa Amaan, Farouk Karim aliwatuliza mashabiki akisema binti huyo ametoroka
hospitali ya vichaa, Kidongo Chekundu na tayari Polisi wamemkamata na kumrejesha
huko.
Hadi dakika
90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 na ndipo zikaongezwa
dakika 30.
Gaudence
Exavery Mwaikimba aliipatia Azam bao la ushindi dakika ya pili tu tangu kuanza
kwa muda wa nyongeza baada ya kuwazidi nguvu na maarifa mabeki wa
Tusker.
Kikosi cha
Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika,
Joackins Atudo, Kipre Balou, Humphrey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba,
Brian Umony/Malika Ndeule dk126 na Uhuru Suleiman/Seif Abdallah
dk64.
Tusker FC;
Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Bright Jeremiah, Martin Kizza, Joseph Shikokoti,
Frederick Onyango/Mark Ochiambo dk93, Andrew Tolowa/Edwin Ombasa dk 55, Khalid
Aucho/Benson Amianda dk 80, Jesse Were/Andrew Sekayambya dk54, Ismail
Dunga/Michael Olunga dk52 na Robert
Post a Comment