Jumla ya
Shilingi Bilioni 12 zimetumika kutekeleza Miradi ya Maendeleo 820
inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeo ya Jamii TASAF kwa Awamu ya Pili ya
Mfuko huo Unguja na Pemba. Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamo
wa Pili wa Rais Khalid Suleiman ameyasema hayo leo katika Warsha ya siku
mbili ya kuwajengea uelewa wa Awamu ya Tatu ya TASAF juu ya ‘Mpango wa
Taifa wa kunusuru Kaya Maskini’ kwa Wajumbe wa Kamati za uongozi na
menejiment za TASAF –Zanzibar huko...
Amesema
katika Miradi hiyo jumala ya Miradi 433 imetekelezwa kwa upande wa
Unguja na Pemba imetekelezwa 387 ambapo Wananchi wa Zanzibar kwa ujumla
wao waliweza kuchangia Shilingi Bilioni 1.3 za Miradi hiyo.
Aidha
amefahamisha kuwa Zanzibar kwa ujumla iilifanya vyema katika kutekeleza
Miradi hiyo licha ya changamoto mbalimbali zilizojitekeza kwa kipindi
hicho cha Awamu ya pili ya TASAF.
Akifungua
Warsha hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd
amewataka wasimamizi wa TASAF kuhakikisha kuwa Fedha zinazotolewa kwa
ajili ya miradi hiyo zinatumika ipasavyo ili kutimiza maelengo ya Mfuko
huo.
Amesema
licha ya Zanzibar kufanya vyema katika Awamu ya Pili ya TASAF viongozi
hao wanapaswa kuyaendeleza mema yote yaliyofanywa katika Awamu mpya
ikiwa ni pamoja na kuziba mianya yote ya ubadhirifu wa pesa za miradi
hiyo.
Balozi
Seif ameongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na azma
yake ya kuunga mkono utekelezaji wa Mpango huo katika Shehia za Unguja
na Pemba ili kuondoa umasikini kwa manufaa ya Jamii na Taifa kwa ujumla.
Amefahamisha
kuwa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini utaimarisha uwazi, uwajibikaji
na kutoa fursa kwa makundi mbalimbali kushiriki kwa kutumia mfumo
madhubuti wa kubaini Walengwa katika Shehia.
Balozi
Seif amewataka Washiriki wa Semina hiyo kushiriki kikamilifu na kuwa
makini ili kufahamu vyema taratibu na miongozo ya utekelezaji wa Awamu
hiyo ya Tatu ya Mfuko huo na hatimaye kufanyia kazi kikamilifu.
Awali
akitoa Shukrani zake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga
ameishukuru Serikali na Wananchi kwa ujumla kutokana na ushirikiano
walioutoa katika Awamu zilizopita na kuomba mashirikiano hayo
yaendelezwe kwa Awamu ya Tatu.
Aidha
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Juma Kassim Tindwa akitoa shukrani kwa
niaba ya Washiriki amemuahidi Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif kuwa
watatumia uwezo wao wote kuhakikisha Miradi ya maendeleo ya TASAF
inasimamiwa vyema na kufikia lengo lililokusudiwa.
Warsha
hiyo ya TASAF Awamu ya Tatu inaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Abdallah Mwinyi na kuwashirikisha Wakuu wa Mikoa ya Unguja na
Pemba,Wakuu wa Wilaya na Menejiment za TASAF –Zanzibar ambapo mada
mbalimbali zitawasilishwa kuwajengea uwezo viongozi hao kuhusu awamu
hiyo Mpya.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 22/01/2013
Post a Comment