Mwili wa Marehemu Yusuph Salum almaarufu kama "Mzee wa Unyago wa Bure" ukitoka nyumbani kwake maeneo ya Mbagala Moringe kuelekea msikitini kwa swala maalum.
Mwili wa Marehemu Yusuph Salum almaarufu kama "Mzee wa Unyago wa Bure" ukiiingizwa katika nyumba yake ya milele. Mzee Unyago wa Bure alikuwa ni kiongozi wa CCM mwanzilishi wa CCM wa matawi ya Mbagala na Moringe kwa nafasi tofauti tofauti katika vipindi tofauti tofauti
Mwili wa Marehemu Yusuph Salum almaarufu kama "Mzee wa Unyago wa Bure" ukifukiwa ardhini. Mazishi yake yalifanyika Mbagala Kongowe
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Temeke, Emmanuel John (Mwenye fulana ya njano) akishiriki vyema kwenye zoezi la kufukia kaburi la Mzee Unyago wa Bure.
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema akiongea machache kwa niaba ya chama cha Mapinduzi ambacho Marehemu alikitumikia katika enzi zote za uhai wake.
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema akitoa ubani wa CCM kwa Rajabu Unyago ambaye ni Mtoto wa Marehemu kwa niaba ya chama.
Umati uliojitokeza kumzika Mzee Unyago wa Bure
Post a Comment