Mhe. Mwanaidi Maajar akilakiwa na
Balozi wa Nigeria nchini Marekani, Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye siku ya
Jumapili January 6, 2013 alipomkaribisha chakula cha jioni maalum kwa
ajili ya kumuaga Balozi wa Tanzania nchini Marekani ambaye anamaliza
muda wake.
Balozi wa Botswana nchini Marekani Mhe. Tebelelo Seretse (kushoto) akiongea jambo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar.
Mke wa Balozi wa Nigeria
akisalimiana na kumkaribisha Mhe. Mwanaidi Maajar huku mumewe Bwn.
Shariff Maajar akiwa amesimama kwenye ngazi akiangalia.
Balozi
wa Nigeria nchini Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye (kulia)
akisalimiana na Mume wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico,
Bwn. Shariff Maajar.
Balozi
wa Nigeria nchini Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye akisalimiana na
kumkaribisha Balozi wa Botswana nchini Marekani Mhe. Tebelelo Seretse nyumbani kwake Potomac, Maryland siku
ya Jumapili January 6, 2013 alipomualika chakula cha jioni maalum kwa
ajili ya kumuaga Balozi wetu ambaye anamaliza muda wake.
Balozi na mumewe Bwn. Shariff
Maajar wakisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn Idd
Sandaly ambaye pia aliongozana na mkewe (wakwanza kushoto) kwenye
chakula cha jioni alichoandaliwa Balozi wetu na Balozi wa Nigeria kwa
ajili ya kumuaga siku ya Jumapili January 6, 2013 nyumbani kwake
Potomac, Maryland.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani
na Mexico Mhe. Mwanaidi Maajar (wapili toka kulia)akiingia nyumbani kwa
Balozi wa Nigeria (hayupo pichani) Potomac, Maryland, huku wakipokelewa
na afisa ubalozi wa Nigeria (wa kwanza kulia) anayesalimia ni mama Lily
Munanka ambaye ni mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani akifuatiwa na mume wa Balozi, Bwn. Shariff Maajar siku ya
Jumapili January 6, 2013 siku Balozi wa Nigeria alipomfanyia chakula cha
jioni maalum kwa ajili ya kumuaga Balozi wetu ambaye anamaliza muda
wake.
Wakati wa chakula.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala
na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, mama Lily
Munanka, Mke wa Balozi wa Zimbabwe, Balozi wa Zimbabwe nchini Marekani,
Mhe. Dr. Machivenyika Mapuranga na Balozi wa Benin nchini Marekani Mhe.
Cyrille S. Oguin.
Kutoka kushoo ni Rais wa Jumuiya
ya Watanzania DMV akiwa pamoja na mkewe, Balozi wa Benin nchini Marekani
Mhe.Cyrille S. Oguin katika picha ya pamoja na Balozi wa Nigeria nchini
Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye.
Post a Comment