|
Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni
Waziri wa Afya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji
akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo
asubuhi. |
CHAMA cha
Wananchi CUF kesho kitafanya Mkutano wake wa hadhara ikiwemo kuwakumbuka wahanga
waliofarikidunia kwenye vurugu zilizotokea Zanzibar na jijini Dar es salaam
mnamo mwaka 2001 wakitetea haki.Akizungumza na waandishi
wa habari kwenye ofisi za CUF wilaya ya Nyamagana Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF
Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
Juma Duni Haji alisema kwamba vyama vya siasa vilivyopo nchini havina budi
kushirikiana ili kuiondoa CCM madarakani."Bila
kushirikiana hivi vyama vya upinzani na ikiwa kila kimoja ni kutaka kuingia
ikulu kivyake basi itakuwa ni ndoto ya kukiondoa madarakani chama tawala (CCM)
ambacho kinashikilia dola" alisema mjumbe huyo.
Haji 'Babu' alisema kwamba Chama
kinachohamasisha na kuchochea vurugu kitambue kuwa siyo njia ya kukiwezesha
chama hicho cha siasa (Upinzani) kuingia ikulu pia hakitaungwa mkono na wananchi
kwani kwa kufanya hivyo wananchi hawatapata ujumbe na sera nzuri wanazopaswa
kuzisikiliza kwenya mikutano ya hadahra ili kufanya uamuzi sahihi wa nani
wachaguliwe kuwaongoza kupitia chaguzi mbalimbali. Hata
hivyo ameonya kuwa hatopenda kuona wafuasi wa vyama vingine watakao fika kwenye
mkutano huo wa hadhara na kufanya fujo, watambuwe kuwa CUF ni chama makini
kilicho na ujasiri wa vurugu lakini kwa sasa hakikusudii kufanya vurugu bali
kiko kwaajili ya kuzitangaza sera na mikakati madhubuti ambayo itakiwezesha
chama hicho kuungwa mkono kwa kupata wanachama wapya ili kuweza kushinda
uchaguzi 2015.Aidha Chama cha CUF kimejipanga
kujiimarisha zaidi kwa kupata wabunge wengi kwenye uchaguzi ujao nchini ili
kuwezesha kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa kama ilivyo
Zanzibar.
|
Sehemu ya wandishi wa habari waliohudhuria kikao
cha mazungumzo na Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF
Taifa. |
|
Na ujumbe
ulihusishwa. |
|
Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni
Waziri wa Afya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji
akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo
asubuhi. |
|
Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni
Waziri wa Afya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji
akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi. |
on Saturday, January 26, 2013
Post a Comment