Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KINANA,MIGIRO, NAPE WAGONGA MCHELE NYAMA CHOMA SARANDA WAKIENDA KIGOMA KWA TRENI

 



Msafara wa Baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahaman Kinana kuelekea Mkoani Kigoma katika maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi umefika salama Mkoani Tabora usiku huu na kupata Mapokezi makubwa kutoka kwa wana CCM mkoani hapo.



Msafara huo ulio na Wajumbe hao wane wa Sekretarieti ya CCM, na wanahabari pamoja na maofisa kadhaa wa Chama hicho ulianza safari yake jijini Dar es Salaam Januari 25, 2013 majira ya saa 8:30 jioni na kusafiri usiku mzima njiani hadi kufika Mjini Tabora majira ya saa moja na nusu 1:30 Usiku.



Mapema mchana msafara huo ulipata mapokezi makubwa katika Stewsheni ya Saranda ambapo viongozi hao baada ya kuhutubia wana CCM walijichanganya na abiria wengine kupata chakula cha mchana.



Kinana aliwaambia wenyeji ambao walikuwa wam,eandaa chakula kwaajili yao kuwa watakula kinachouzwa na wakazi wa hapo kuchangia kipato chao kama wasafiri wengine.






Hakuna kujivunga hapa.


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai akimpokea Katibu Mkuu wa CCM.


Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiteremka katika treni.


Katibu Mkuu wa CCM akiongozana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai ambaye ni Mwenyekiti (wapili kulia) na Naibu Katibu Mstaafu, John Chiligati.




Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa Skafu na Chipkizi wa CCM Saranda, Derick Chongole mara baada ya kuwasili eneo hilo.


credits: Father Kidevu


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua mishikaki kwa mmoja wa wauzaji wa vyakula mbalimbali husuasan nyama, baada ya kuwasili na msafara wake stesheni ya Saranda, mkoani Singida, leo mchana. Kinana na msafara wake wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wanasafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam, kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. (Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai. (Picha na Bashir Nkoromo)

Makatibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia) na wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia) wakinunua chakula kwa mamalishe, kwenye stendi ya Saranda mkoani Singida, daaba ya kuwasili kwenye stesheni hiyo, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM.(Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mstaafu John Chiligati wakishiriki kucheza ngoma ya wakazi wa mkoa wa Singida, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Martine Shigela.(Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipuliza filimbi kuchangamsha ngoma aliyokuwa akishiriki kucheza na wananchi wa mkoa wa Singida, katika burudani ya ngoma iliyotolewa, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM.(Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu Mkuu wa CCM, akisalimiana na wananchi wa Itigi.




Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wananchi wa Saranda, tarafa ya Kilimatinde, Wananchi wamefurahi kuona viongozi wao wakiwa nao pamoja na kusafiri nao pamoja.
 
Ujumbe wa Sekretarieti ukisalimiana na Uongozi wa Tabora mara baada ya kuwasili hapo wakiwa njiani kuelekea Kigoma kwa kutumia usafiri wa Treni ya Reli ya kati.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top