Magari yakiwa
yanateketea kwa moto mkoani Mtwara.
Nyumba
ikiteketea kwa moto mkoani Mtwara hii leo katika vurugu
zilizozuka.
WATU watatu
wamefariki dunia Mkoani Mtwara baada ya kutokea vurugu kubwa kati ya Askari wa
Jeshi la Polisi na waendesha Pikipiki maarufu (Bodaboda).
Taarifa za
tukio hilo zilizotufikia hivi Punde zinadai kwamba vurugu hizo zimesababishwa na
Askari Poli kumkamata mmoja wa dereva bodaboda hao na kuanza kumpiga kiasi cha
kupoteza fahamu.
Mbali na watu hao
waliouwawa katika vurugu hizo taarifa hiyo pia imeeleza kuwa zaidi ya nyumba na
ofisi tatu za serikali pamoja na magari matano yamechomwa
moto.
Tunaendelea
kuzifuatia taarifa hizo kwa kina na tutaendelea kuwajulisha hivyo endeleeni
kufuatilia kwa undani wake.
Chanza Habarimpya.com

1 comments:
JAMANI SASA IMEFIKA WAKATI SERIKALI IFANYE MAZUNGUMZO NA WANANCHI HUSUSANI KWA MIRADI YOTE INAYOHUSU MAKAZI YA WANANCHI KAMA HUU WA GESI,HEBU TUFIKIRIE WENZETU WALIOFARIKI KISA WANALILIA MAENDELEO YAO KWA MALI MUNGU ALIOIJALIA NCHI YETU ILI IMUNUFAISHE KILA MTANZANIA TENA WA ENEO HUSIKA LAKINI KIFO KWANZA?HII DAMU YA WATANZANIA INAMWAGIKA MPAKA LINI?JE YAWEZEKANA MWENYE SHAMBA KULALA NJAA INGALI SHAMBANI MWAKE KUNA MAZAO AMBAYO YANAVUNWA NA KUPELEKEWA JIRANI KISA YEYE HANA UJUZI WA KUYAVUNA?TENA AAMBIWE FAIDA BAADAE ILA ENDELEA KUVUMILIA!HIZI NI ZAMA ZA UKWELI NA UWAZI VIONGOZI ELIMU MNAYO FANYENI JUHUDI ZOTE MUWATIMIZIE HAWA NDUGU ZETU HAJA ZAO,NA MUNGU ATABARIKI MRADI HUU.KAMA HAMTAFANYA HIVYO MJUE WAZI NCHI YETU TAYARI IMEINGIA PA BAYA NA AMANI INATUPUNGIA MKONO WA KWA HERI YA KUONANA!MSILAZIMISHE WALA SILAHA HAZIFAI KWA NCHI YETU HII ZAIDI YAPENDENI MAISHA YA WENGI.NENO LA MUNGU LINASEMA MWANAO AKIOMBA MKATE UTAMPA JIWE?NA AKIOMBA SAMAKI UTAMPA NYOKA?SASA VIONGOZI WETU NDANI YA FAMILIA ZENU MNA WATOTO WASIKIVU NA WATUKUTU JE MNAWAADHIBU JE WALE WATUKUTU?JE HAKI YA MTUKUTU INAPUNGUZWA KWA ASILIMIA 90% NA KUMPATIA MSIKIVU?AU UNATAFUTA MBINU ZA KUMREKEBISHA KWA UPENDO WA HALI YA JUU SANA NA KUMPATIA MAHITAJI YAKE VIZURI ILI MIJI YENU IWE NA AMANI!SASA BASI FANYENI HIVYO KWA NDUGU ZETU WA MTWARA ILI NCHI IBAKI NA AMANI TENA ILE AMANI IPITAYO AMANI ZOTE.MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU,MUNGU TUSAMEHE MAKOSA YETU SISI WATANZANIA.
ReplyPost a Comment