* WAAMUA KUIKATAA MOVIE YAKE MPYA
STAA wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ yamemkuta baada ya ile ishu yake ya kutengeneza filamu inayoitwa Sister Marry ambapo mapadri wamemtaka asiipeleke sokoni milele.
Ishu hiyo ilitokea kwenye kikao kizito cha saa 5 kilichofanyika Jumanne iliyopita katika Ofisi za Utamaduni jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa kikao hicho walikuwa Ray, Mkurugenzi Mtendaji wa Utamaduni aliyetajwa kwa jina moja la Mwansoke, mapadri wanne na mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni wa kutoka Ofisi za Usalama wa Taifa.
Kikao hicho kilikuja baada ya hivi karibuni viongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam kumtaka msanii huyo ajieleze kimaandishi ni kwa nini mtawa Sister Marry (Irene Uwoya pichani) alikuwa akifanya matendo ambayo kiuhalisia, Wakatoliki wenyewe huwa hawayafanyi.
Kabla Ray hajajieleza kwa maandishi ndipo alipoitwa huko na kukubaliana ana kwa ana na jopo hilo huku mashinikizo kadhaa yakielekezwa kwake.
Awali, wajumbe wote wakiwa wamekaa kwenye viti, filamu hiyo yenye saa 3 iliwekwa mwanzo mwisho huku mapadri hao wakiguna kila wakati, hasa wakati Sister Marry akiwa anafanya mambo yake mabaya.
Baada ya kumalizika kwa filamu hiyo, hoja zikaanza. Mwansoke akasema vipande vyote vichafu vinyofolewe na kubaki vile ambavyo wajumbe hawakuvigunia.
Baada ya bosi huyo kusema hayo, mapadri wakasema ‘noooo’. Filamu hiyo isiende mitaani hata kidogo kwani imejaa udhalilishaji wa Wakatoliki.
Inasemekana Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Maximilian Kolbe lililopo Mwenge Kijijini (jina halikupatikana mara moja) yeye alipigilia msumari wa mwisho kwa maneno aliyoyatoa.
Alisema kwa kuwa filamu hiyo ilirekodiwa kwenye kanisa lake hilo, anataka vipande vyote vya kanisa hilo vitolewe ndipo iingie mtaani, jambo ambalo lilimtoa machozi Ray.
Ray sasa! Siku ya Alhamisi iliyopita, Ray alizungumza na Amani na kukiri kuwepo kwa kikao hicho. Akasema itakuwa vigumu kuviondoa vipande vya kanisa hilo kwa sababu asilimia 85 ya filamu nzima imerekodiwa Maximilian Kolbe.
“Asilimia 85 ya filamu imerekodiwa Maximilian Kolbe, sasa wanaposema niviondoe ni kuimaliza filamu yote. Filamu ni ya saa 3, ukivitoa vipande vya kanisa si itabaki dakika 5 tu,”alisema Ray.
Alisema kikao kiliisha kwa maamuzi hayo, kwamba mtu wa utamaduni alisema vipande vichafu vinyofolewe huku mapadri wakitaka muvi nzima isiende sokoni na paroko wa Maximilian Kolbe akitaka kanisa lake lisionekane kwenye filamu hiyo.
4 comments
HAYA YOTE NI MATOKEO YA BAADHI YA MAKASISI WA KANISA KATOLIKI KUJISAHAU NA KUACHA MAAGANO WALIOMGANIA MUNGU HUKU WAKIMPIGA MUNGU KISOGO NA KUISHI WANAVYOTAKA HUKU UTUMISHI WAO WAKIHESABU NI KAMA AJIRA YA KAWAIDA.UKWELI BAADHI YA MAPADRI MNATUABISHA SANA HATA KUONA HUDUMA ZENU HAZIFAI KWA TAIFA LA MUNGU,TUNAWAOMBA ANAEONA AMESHINDWA KUMTUMIKIA MUNGU AAGE MAPEMA KABLA YA UHARIBIFU,NA ARUDI URAINI.SISI WAKRISTU WAKATOLOKI TUNAKASHIFIWA SANA PINDI TUKITAMKA PADRI TU UNAPEWA MFANO HAI WA MAOVU YAKE NA MTU YUKO TAYARI AKUPELEKE KWAKE KUKUTHIBITISHIA ANAYOKUELEZA NI KWELI.JAMANI BABA ZETU KUNA NINI DUNIANI?
ReplySASA HILI NDILO DHEHEBU AMBALO MAOVU YANARUHUSIWA AU YANAFUNGIWA MACHO KIASI KWAMBA INAONEKANA SI KANISA LA KIROHO?MATOKEO YAKE WAUMINI WANAHAMIA MADHEHEBU MENGINE HUKU MAPADRI MKITUULIZA TUNAFUATA NINI HUKO MKASAHAU NAE MUNGU ATAWAULIZA ILIKUWAJE HAWA WAKAONDOKA HUMU?CHA AJABU IKIINGIA KANISANI MAHUBIRI KAMA MAELEZO KIASI KWAMBA UKITOKA HUNA MABADILIKO YO YOTE.MAHUBIRI NI YA HARAKA SANA HUKU KUPOTEZEA KUPO KWA SABABU MHUBIRI HUYO ANA HARUFU YA POMBE TENA ANAPEPESUKA SASA KWELI KWELI HIYO NI MISA AU KIKAO?HATA KUKOSOA MAKOSA NA DHAMBI ZETU HAWEZI KWA SABABU KAMA BAR YA POMBE TULIKUWA NAE JANA JIONI(JMOSI)KAMA NYUMBA NDOGO USISEME KWA WANANDOA JE YEYE KASISI INAKUWA NYUMBA GANI?ANAJUA YEYE ALIEYENAYO MPAKA MAJIRANI WANAONA HATA KUKUITA NJOO UMUONE HUYO PADRI WENU NDIYO KAINGIA KWA HUYO CHANGU DOA ANAETUULIA WAUME ZETU!HIVI KWELI KABISA MISA YA KWANZA JPILI ANAIADHIMISHA BILA WOGA!HAYA SASA MAUNGAMO NDIYO SHUGHULI KUBWA NA YAKUCHOSHA MPAKA UNAONA BORA UENDE PAROKIA NYINGINE KULIKONI PALE ULIPO ILI TU USIKUTANE NA PADRI HUO.KASHIFAAAA HAYA HUYO MANEENDA KUUMUNGAMIA ALIKUWA BAA MPAKA SAA 8 USIKU WACHA UPUMBAVU WEWE TULKUWA NAE!HOI HOI HOI!
ReplyJAMANI SISI WAKATOLIKI NI VIPI YAANI HATUJIELEWI KABISAA NA HATUJUI TUFANYE NINI ENDAPO BAADHI YA MAPADRI WANATUABISHA KIASI HIKI MPAKA TUNABAKI TUKIOMBA KIMYA KIMYA NA KUMLILIA MUNGU TU!KILA LEO MAGEZETINI KASHIFA ZA NGONO KWA MAPADRI NA MASISTA NAO WANAFUATA NYUMA.SASA MILANGO YA SHETANI IMEPATA MWANYA MZURI HATA KANISA LINA TUMIKA KWA UCHAFU KAMA HUO WA FILAMU HIYO KUFANIKIA NDANI YA NYUMBA YA MUNGU SEHEMU TAKATIFU!EE MUNGU TUREHEMU WAKATOLIKI MAANA TUNAANGAMIA!
ReplyILA IMENIPASA NIFE MKATOLIKI MAADAMU BIBLIA NAJUA KUISOMA NA SEHEMU PEKEE YA KUONGEA NA MUNGU ANA KWA ANA!
ReplyPost a Comment