Kundi la wananchi
wanaodaiwa kuwa na hasira, wamevamia kituo cha Polisi cha Kibiti Wilayani Rufiji
na kufanya vurugu kubwa baada ya raia mmoja kufa kwa kile kilichodaiwa kipigo
cha Polisi.
Chanzo chetu cha Habari
kutoka Kibiti kinaipasha kuwa kijana aliyefariki kutokana na kipigo hicho ni
Hamis Mpondi, ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya
Muhimbili.
Habari zaidi zinapasha kuwa
hivi sasa wananchi hao wanaendelea kuteketeza nyumba za Askari Polisi hao
zilizopo jirani na kituo hicho, licha ya Polisi kuendelea kufanya juhudi za
kuwatawanya kwa mabomu katika eneo hilo.
Aidha wananchi hao wameanza
kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe,
magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha
Polisi Kibiti.
Hali inaelezwa kuwa inazidi
kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo
kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu. Vurugu
zinaendelea, Habari kwa hisani ya Father Kidevu

Post a Comment