BAADA YA KUWA TANZANIA
KWA KIPINDI CHA MIAKA 82, TOKA ENZI ZA BOAC, SHIRIKA LA NDEGE LA UINGEREZA YAANI
BRITISH AIRWAYS LIMEAMUA KUITOSA RASMI TANZANIA,GLOBU YA JAMII INAWEZA
KUTHIBITISHA!
HABARI ZA UHAKIKA TOKA
JIKONI ZINASEMA NDEGE YA MWISHO YA BRITISH AIRWAYS KUTUA TANZANIA ITAKUWA MACHI
29, 2013 WAKATI BOEING 767 YA SHIRIKA HILO AMBAYO NI KIJEBA (ZINAZOKUJA HUKU
ZINA UMRI ZAIDI YA MIAKA 20) ITATUA KWA MARA YA MWISHO.
NA KWA HUZUNI KUBWA KWA
WADAU WAKE, OFISI ZA BRITISH AIRWAYS PALE SERENA INN JIJINI DAR ES SALAAM
ZITAPIGWA KUFULI RASMI MACHI 31, 2013
Post a Comment