MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, DCI, Robert Manumba, amepelekwa
Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Habari za uhakika zilizoifikia Tanzania Daima na kuthibitishwa na msemaji wa jeshi hilo Advera Senso zimeeleza kwamba Manumba alisafirishwa kwa ndege maalumu ya kampuni ya AAR kwenda Afrika Kusini akitokea hospitali ya Agakhan ya jijini Dar alikokuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Hata hivyo, Senso hakutaja hospitali alikopelekwa, bali alidai kwamba atatibiwa katika moja ya taasisi za tiba mashuhuri nchini humo.
Hali ya Manumba, ilibadilika na kuwa tete kwa siku kadhaa na kufikia hatua ya kuvumishwa kwamba amefariki.
Hata hivyo, DCI Manumba alilazwa katika Hospitali ya Agakhan ya jijini Dar es Salaam ambako hali yake ilikuwa ikiriporiwa kuwa mbaya.
Manumba amekuwa akipumua kwa kusaidiwa na mashine kwa zaidi ya siku nne, na taarifa za ndani za jeshi hilo zilisema amekuwa akisumbuliwa na malaria kali ambayo imeathiri utendaji kazi kwa kiwango kikubwa katika mwili wake.
Chanzo: Tanzania Daima

Post a Comment