Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JK AKIRI NISHATI BADO NI TATIZO

RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa Tanzania bado inakabiliwa na changamoto ya uwezo katika sekta ya nishati ambayo ni muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi na wananchi wake kwa ujumla.
Kikwete amesema hayo wakati anachangia katika mjadala maalumu kuhusu uhamasishaji wa sekta binafsi katika kuwekeza kwenye sekta ya nishati barani Afrika ambao umeongozwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na kuratibiwa na kiongozi wake, Rajiv Shah.
“Uwezo wa kuzalisha na kuusambaza bado ni changamoto kwetu, tunataka kuacha kutegemea umeme we maji pekee na kuanza kuzalisha kwa njia zingine mbadala, lakini bado uwezo wetu kama serikali ni mdogo na tumeamua kuwashirikisha watu binafsi ili umeme huu uweze kuwafikia wananchi walio wengi zaidi,” alisema.
Rais Kikwete yuko mjini Davos, Uswisi kuhudhuria kikao cha kila mwaka cha uchumi ambapo viongozi mbalimbali wa nchi, wakurugenzi wa mashirika na makampuni makubwa duniani huhudhuria kwa ajili ya kujadili changamoto, matumaini na mapendekezo kadhaa kwa lengo la kukuza na kuimarisha uchumi duniani.
Kikao chicho pia kimehudhuriwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Haile Mariam Desalegne na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB), Donald Kaberuka.
Katika kikao kingine ambacho kimehusu kilimo na usalama wa chakula barani Afrika, Rais Kikwete alisema Tanzania imetengeneza mkakati maalumu kuhusu kilimo ambao unatekelezwa kama ulivyopangwa.
Alisema pia kuwa kumekuwa na upotoshwaji kuhusu uwekezaji mkubwa katika kilimo ambao umetafsiriwa Kama uporaji wa ardhi ya wananchi.
“Tanzania tunayo ardhi, na ile tunayotoa kwa wakulima wakubwa ni ardhi iliyotengwa na serikali kwa ajili ya wakulima wakubwa (land bank),” alisema.
Rais Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa nchi na wa makampuni binafsi waliopo Davos kwa ajili ya mkutano wa uchumi.
Pia alipata fursa ya kuzungumza katika chakula maalumu kilichoandaliwa na Shirika la Roll Back Malaria ambapo washiriki walizungumzia suala la diplomasia na afya.
Katika hilo, Rais Kikwete alisema serikali pekee haziwezi kutatua changamoto za afya, hivyo zinahitajika pia juhudi za nchi rafiki na mashirika binafsi.
“Tunahitaji kuimarisha huu uhusiano na kuendelea kufanya kazi pamoja kwani serikali zinahitaji sana wenza katika kutatua changamoto nyingi zilizopo katika sekta ya afya kwani kunahitajika nguvu zaidi ya zile za serikali,” alisisitiza.

Chanzo: Freemedia
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top