Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DHAMANA YA LULU KUANZA KUSIKILIZWA IJUMAA

Mahakama ya kanda ya Dar es Salaam, itaanza kulisikiliza rasmi  ombi la msanii wa Filamu nchini, Elizabeth Michael Januari 25 mwaka huu.

Elizabeth ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Lulu, anatuhumiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba April 7 mwaka jana.

Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe la leo, kesi itasikilizwa kwa Jaji Zainabu Mruke, na ombi la kusikilizwa kwa dhamana hiyo limetoka kwa mawakili wa Lulu ambao ni Peter Kibatala, kenedy Fungamtama na Massawe Fulgence.
Hati ya ombi hilo inaonesha kwamba wanawasilisha chini ya kifungu 148(1) na (2) Sheria ya cha makosa ya jinai ya mwaka 2002.

Mawakili hao wamedai kwamba kosa la mtuhumiwa linaweza kupatiwa dhamana iwapo atatimiza masharti yatakayotolewa na hakimu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top