Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kati Vuai
Mwinyi,alipowasili katika shere za Ufunguzi wa Jengo la
Chuo cha Utumishi wa Umma,liliopo Tunguu,Wilaya ya Kati
Unguja,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi
Matukufu yaZanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa
jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa
Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49
ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Utumumishi
wa Umma na Utawala Bora HajiOmar Kheir.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo
cha Utumishi wa Umma,(IPA) Harusi Masheko
Ali,alipotembelea madarasa ya kusomea,baada ya ufunguzi rasmi
wa Jengo la Chuo hicho uliofanyika jana Tunguu, Wilaya ya
Unguja, katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein,(wa pili kulia) akifuatana na Waziri
wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir,(kushoto)
pamoja na Viongozi wengine baada ua kulifungua jengo la Chuo
cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
jana,katika shamra shamraza kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar
Baadhi
ya Viongozi na Wananchi walioalikwa katika sherehe za
Ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,zilizofayika
jana huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja,wakimsikiliza kwa makini
mgeni rasmi Rais wa Zanzibar,alipokuwa akitoa hutuba yake
katika kusherehekea shamra shamra za Miaka 49 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi
ya Viongozi na Wananchi walioalikwa katika sherehe za
Ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,zilizofayika
jana huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja,wakimsikiliza kwa makini
mgeni rasmi Rais wa Zanzibar,alipokuwa akitoa hutuba yake
katika kusherehekea shamra shamra za Miaka 49 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiwahutubia Wananchi, katika
sherehe za ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi
wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika
shamra shamraza kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali
Iddi,Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Maalim Abdalla Suleiman,(wa
pili Kulia) na Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora
Haji Omar Kheir,(kushoto) .Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein ametowa wito wa Taasisi
za Serikali na Taasisi Binafsi kukitumia Chuo cha Utawala wa Umma ili kuwajengea
uwezo wafanyakazi wao kwa manufaa ya Taifa.
Amesema kuwa Chuo
hicho kitaweza kuwajengea uwezo ujuzi ubunifu uwandilifu na kuweza kuwa
watumishi bora wa taifa na jamii kwa ujumla . Hayo aliyasema leo huko
Tunguu Mkoa wa kusini Unguja wakati alipokuwa akifungua Jengo Jipya la Chuo cha
Utawala wa Umma ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za sherehe ya miaka 49
ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Amesema kuwa madhumuni
makubwa yakujenga vyuo hivyo ni kuleta mabadiliko yenye lengo la kupata ustawi
bora wa maisha kwa Wazanzibar na kuwa na wafanyakazi wenye taaluma inayostahiki
.
Pia
amesema kuwa chuo hicho kitaweza kutowa wanafunzi waliobora wenye misingi imara
ya utawala bora na kuweza kujua haki na majukumu ya kazi
zao. Aidha Dkt Shein ameuomba uwongozi kujitahidi kuwa na
wakufunzi ambao wataofundisha katika chuo hicho kuwa na sifa zinazokubalika ili
chuo hicho kiweze kutoa wanafunzi bora .
Halikadhalika
aliutaka uwongozi kuwajengea mazingira mazuri wakufunzi wa chuo hicho ili
wasiweze kuvunjika nguvu katika utendaji wa kazi zao . Jumla ya
shilling bilioni 1milioni mia moja na saba tayari zimeshatumika mpaka sasa kwa
ajili ya Ujenzi huo na hivi sasa zinahitajika shilingi milioni elfu 3 kuweza
kuinua Jengo hilo kuwa la ghorofa moja. Jengo la chuo hicho linatarajiwa kuwa na
sehemu nyengine mbali mbali zikiwemo za kuegesha magari,mkahawa, mabweni na
uwanja wa michezo .


Post a Comment