Timu ya Young Africans
Sports Club imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Arminia Bielefeld ya
Ujerumani katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo jioni katika uwanja wa Adora
Football pemebni kidogo ya mji wa Antalya.
Armini Bielefeld ilianza
soka kwa kasi kwa lengo la kujipatia bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa
Yanga na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' ilikuwa kikwazo kwao kwani
mashambulizi yao yaliishia mikononi mwake.
Ikiwa ni mchezo wake wa
kwanza wa kujipima nguvu Young African iliweza kuonyesha soka safi katika
kipindi cha kwanza hali iliyowashangaza wajerumani hao na kipindi cha pili
kuamua kufanya mabadiliko ya kikosi kizima.
Viungo wa Yanga Frank
Domayo, Haruna Niyonzima na Kabange Twite waliweza kutawala mchezo kwa dakika 45
zote za kipindi cha kwanza huku baadhi ya wajerumani waliokuwa wakishuhudia
mchezo huo kushangazwa na kiwango cha timu ya Yanga
Hadi mapumziko timu zote
zilikwenda mapumziko , Young Africans 0 - Arminia Bielefeld.
Kipindi cha pili Arminia
Bielefeld iliamua kubadilisha kikosi chake chote cha wachezaji kwa lengo la
kuingiza nguvu mpya ili waweze kuikabili kasi ya wachezaji wa Yanga ambao
walionekana kuwa imara na bora zaidi.
Dakika ya 55 Yanga ilifanya
mabadiliko kwa kuwatoa Said Bahanuzi na David Luhende na nafasi zao kuchukuliwa
na Jerson Tegete na Saimon Msuva.
Jerson Tegete aliipatia
Young Africans bao la kwanza dakika ya 60 ya mchezo, akiunganisha pasi safi
aliypewa na Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Arminia Bielefeld na kumpa pasi
Tegete ambaye aliukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao la
kwanza.
Kuona hivyo wajerumani
walikuja juu kusaka bao la kusawazisha, lakini bado ukuta wa Yanga uliendelea
kuonekana kuwa makini lakini makosa ya mshika kibendera yaliipelekea Armini
Bielefeld kupata bao la kusawazsiha dakika ya 81 kupitia kwa Eric Agyemang
amabaye alikua ameotea.
Mpaka dakika 90 za mchezo
zinamalizika Young Africans 1 - 1 Armini Bielefeld.
Kocha Mkuu wa Young
Africans Ernest Brandts amesema amefurahishwa na kiwango walichokionyesha
wachezaji wake na anaamini kadri siku zinavyokwenda wanazidi kuimarika na kuwa
bora, hivyo katika michezo mingine wataendelea kuonyesha mabadiliko
makubwa.
Young Africans: Ally
Mustafa 'Barthez, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin
Yondani, Kabange Twite, Haruna Niyonzima/Nizar Khalfan, Frank Domayo/Nurdin
Bakari, Said Bahanuzi/Jerson Tegete, Didier Kavumbagu, David Luhende/Saimon
Msuva

Post a Comment