Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mwinyihaji Makame Mwadini
ameishukuru Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo JICA kwa
kusaidia Maji safi na salama katika Visiwa vya Unguja na
Pemba..
Amesema Serikali
imefarajika kuona Vijiji mbali mbali vya Unguja na Pemba vinafaidika na Miradi
hiyo chini ya ufadhili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na
Japan.
Akizinduwa Mradi wa Maji
Safi na Salama huko Fumba Dkt Mwinyihaji amewataka Wananchi hao kuendelea
kushirikiana katika utekelezaj iwa Miradi ya Maendeleo ili kutekeleza kwa
vitendo malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar. ya mwaka 1964.
Amesema ushirikiano
waliouonesha katika utekelezaji wa Mradi huo ni wakupigiwa mfano,hivyo hakuna
sababu yakubaguwana katika Miradi ianayo waletea tija ikiwemo ya Afya,Elimu na
ya kiuchumi.
Mradi wa Maji Safi na
Salama wa Fumba umeanza utekelezaji wake mwaka 2009 na umegharimu kiasi cha
shillini millioni Mia Moja na 29 zilizotolewa na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na Serikali ya Japan


Post a Comment