Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein
amemteuwa Mussa Msheba Suleiman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usafiri wa
Barabarani katika Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano,Zanzibar.
Kwa
mujibu wa Taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu
Mkuu Kiongozi ,Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa Rais amefanya
uteuzi huo kwa mujibu ya uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 14((2)(a)
cha sheria ya Usafiri wa Barabarani(THE ROAD TRANSPORT ACT)Namba 7ya
mwaka 2003.
Uteuzi huo umeanza tarehe 06 Januarri,2013.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIOBAR.
13/1/2013.
Post a Comment