Mtangazaji wa Clouds FM, Shaffih Dauda (kulia) akiwa ameshikilia fomu ya kuwania nafasi ya ujumbe katika uchaguzi mkuu wa TFF leo |
WADAU 19
wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika
Februari 24 mwaka huu.
Fomu hizo zimeanza kutolewa leo (Januari 14 mwaka huu) ambapo wawili
wamechukua nafasi ya Makamu wa Rais wakati waliobaki wanaomba ujumbe wa
Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.
Waliochukua fomu za umakamu wa rais ni Wallace Karia na Ramadhan Nassib.
Wote ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF inayomaliza muda wake.
Waliochukua fomu za ujumbe ni Shaffih Dauda, Athuman Kambi, Hussein
Mwamba, Stewart Masima, Yusuph Kitumbo, Mugisha Galibona, Vedastus
Lufano, Twahili Njoki, Charles Mugondo, Elley Mbise, Farid Nahdi, Ayubu
Nyaulingo, Nazarius Kilungeja, Epaphra Swai, Khalid Abdallah, James
Mhagama na Selemani Bandiho.
Post a Comment