Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia ubani kama
ishara ya ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)
yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka
hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya
Kiislamu.
Ustadh Rashid Jaffer wa
Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa
Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini
Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu
ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Ustadh Abdulla Hamad wa
Chuo cha Kiislamu,akitoa tafsiri ya Aya za Quran,zilizosomwa na Ustadh Rashid
Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya
Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya
Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na
kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Mtafsiri Lugha kwa njia ya
alama akitoa tafsiri ya maneno yanayozungumzwa wakati wa Hafla ya sherehe za
Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika
viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Wake za Viongozi na
Akinamama wakisikiliza Maulid Barzanj ya Kuzaliwa kwa yaliyosomwa na wasomaji
mbali mbali na Qasida katika sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume
Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini
Zanzibar.
Baadhi ya Waumini wa Dini
ya Kiislamu waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume
Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini
Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia)
akitiwa Marashi wakati wa kumswalia Mtume (S.A.W) wakati wa sherehe ya Maulid ya
Kuzaliwa kwake katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na
Viongozi wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar,alipowasili katika viwanja vya
Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W)
yaliyofanyika jana.
Ustadh Ali Twalib
Mohamed,wa Kibanda Hatari Mjini Zanzibar akisoma Maulid Barzanj Mlango wa kwanza
katika kusherehekea kwa kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika
jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya
Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W)
yaliyofanyika jana, na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid
Karume,(katikati).
Wanafunzi wa Madrasa
Munawara Shaurimoyo Wilaya ya Mjini Zanzibar wakisoma Qaswida ya Mwaka 1434 el
Hijra,wakati wa sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)
yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisra Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi
kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji
Khamis,iliyotayarishwa na jumuiya hiyo katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa
Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini
Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji
Khamis,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya
kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
source matukio issa
michuzi
Post a Comment