MKURUGENZI wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai nchini Tanzania,Robert Manumba amezidiwa kiasi cha kupumua
kwa msaada wa mashine katika Hospitali ya Aga Khan.
Habari zilizopatikana hivi punde zinaeleza kuwa
Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa,
ikiwamo figo.
Taarifa
za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa
hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo
zake zote mbili kushindwa kufanya
kazi.
Manumba amelazwa katika
wodi ya wagonjwa mahututuzi (ICU) kwa ajili ya uangalizi wa jopo la
madaktari,taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilizoifikia BLOG
HII zinadai kwamba
Mkurugenzi huyo wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania amezidiwa kiasi cha kupumua
kwa kutumia mashine ya hewa safi ya Oxgen.
Habari zilizopatikana
jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na
maradhi kadhaa, ikiwamo figo,taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana
kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na
hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya
kazi.
“Alitakiwa kupelekwa nje
ya nchi kwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu
kumzindua, ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi
hilo. Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso,
alithibitisha kamishna huyo kulazwa ICU Aga
Khan.
“Ni kweli amelazwa
katika hospitali ya Aga Khan, lakini hali yake inaendelea vizuri,” alisema
Senso.
Mtu wa karibu na
Manumba, alisema, Manumba alikutwa na vijidudu 500 vya malaria, tatizo ambalo
lilisababisha pia viungo vyake vingi, ikiwamo figo kushindwa kufanya
kazi.
Daktari Mganga Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Dk
Jaffer Dharsee alisema jana kwamba Manumba alifikishwa katika hospitali hiyo
tangu juzi akisumbuliwa na malaria na alikuwa
hajitambui.
“Nimepigiwa simu nyingi
leo (jana), nikiulizwa na watu mbalimbali wakitaka kufahamu kama Manumba
amefariki dunia, ninachotaka kuwaambia ni kwamba ni mzima lakini yuko mahututi
ICU"alisema Dk Dharsee.
MKURUGENZI wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai nchini Tanzania,Robert Manumba amezidiwa kiasi cha kupumua
kwa msaada wa mashine katika Hospitali ya Aga Khan.
Habari zilizopatikana hivi punde zinaeleza kuwa
Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa,
ikiwamo figo.
Taarifa
za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa
hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo
zake zote mbili kushindwa kufanya
kazi.
Manumba amelazwa katika
wodi ya wagonjwa mahututuzi (ICU) kwa ajili ya uangalizi wa jopo la
madaktari,taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilizoifikia BLOG
HII zinadai kwamba
Mkurugenzi huyo wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania amezidiwa kiasi cha kupumua
kwa kutumia mashine ya hewa safi ya Oxgen.
Habari zilizopatikana
jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na
maradhi kadhaa, ikiwamo figo,taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana
kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na
hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya
kazi.
“Alitakiwa kupelekwa nje
ya nchi kwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu
kumzindua, ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi
hilo. Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso,
alithibitisha kamishna huyo kulazwa ICU Aga
Khan.
“Ni kweli amelazwa
katika hospitali ya Aga Khan, lakini hali yake inaendelea vizuri,” alisema
Senso.
Mtu wa karibu na Manumba, alisema, Manumba alikutwa na vijidudu 500 vya malaria, tatizo ambalo lilisababisha pia viungo vyake vingi, ikiwamo figo kushindwa kufanya kazi.

Post a Comment