Mkurugenzi wa habari nchini Habi Gunze amesema Vituo vya Redio
ambavyo ni chochezi, vitachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na
kuvifugia.
Gunze ametoa kauli hiyo juzi, mada mfupi uliopita mara baada
yakupokea taarifa fupi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo,
kufuatia Kamatia ya Bunge iliyozuru Mkoani humo .
Gunze amesema vituo ambavyo huenda vikafungiwa ni pamoja na vile
vinavyo eneza na kufanya uchochezi wa waumini wao kwakutumia mwamvuli wa
dini.
Awali akitoa taarifa Mbele ya kamati ya Bunge
inayoshughullikia huduma za jamii Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema katika siku za
hivi karibuni kituo cha Kwa Neema Fm cha jijini Mwanza na kile cha Redio Imani
kilichopo Mkoani Morogoro vimekuwa vikienda kinyume na utaratibu na hivyo kuweka
rehani Amani ya Nchi.
Akizungumzia kuhusu Kwa Neema Fm amesema, kituo hicho kimekuwa
kikirusha matangazo yake nakuwashawishi Wakristo kuchinja nyama, badala
yakuwapelekea wenzao waislamu.
Kwa upande mwingine Ndikilo amesema, kituo cha Redio Imani kilitumika
vibaya wakati azoezi la Sensa ya watu na maakazi ilyofanyika nchini kote Agosti
26 mwaka jana wa 2012.
Kamati ya
Bunge kuhusu huduma za jamii ipo Mkoani Mwanza kwa Ziara ambapo
pamoja na mambo mengine itatembelea chuo cha Michezo Malya, Vituo vya Redio Free
Afrika na Star TV pamoja naTBC Mwanza.
NA
ATLEY KUNI- AFISA
HABARI
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza
Post a Comment