|
Afisa wa Magereza
wa Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam, Gibson Mwakibibi akiwaonyesha mfuniko
wa Hotpot (Chombo cha kuhifadhia chakula) pamoja na Radio Kamati ya Bunge ya
Ulinzi na Usalama ambapo vifaa hivyo vinatumika kuficha simu, visu, bangi na
vifaa mbalimbali ambavyo ni hatari kwa usalama wa Mahabusu na wafungwa. Vifaa
hivyo vilikuwa vinaingizwa na mahabusu hao pmaoja na baadhi ya ndugu zao
wanapopeleka chakula gerezani hapo. Hata hivyo, maafisa magereza kwa kutumia chombo
cha kugundulia vifaa mbalimbali (Metal Detector) kinachotumika gerezani hapo huvikamata
vifaa hivyo.
|
|
Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu pamoja na wajumbe wa
kamati yake wakiwauliza maswali mbalimbali Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza katika Gereza la Segerea lililopo jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilitembelea
sehemu wanapolala Wafungwa na Mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na
kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.
|
|
Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala,
Mussa Azzan Zungu akizungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Segerea
jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati kamati yake ilipofanya ziara ya
kikazi katika gereza hilo jana. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala
wafungwa na mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa
wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa
|
on Saturday, January 19, 2013
Post a Comment