Waziri wa uchukuzi Dk.
Harryson Mwakyembe(pichani), ameuagiza uongozi wa mamlaka ya bandari nchini TPA
kutoa taarifa na kumfichua mtu yoyote ndani ya mamlaka hiyo aliyekwamisha
mkataba wa ujenzi wa mtambo wa upakuaji wa mafuta SPM wenye uwezo wa kupakua
zaidi ya lita 100,000 za mafuta kwa siku.
Sambamba na hilo
ameiagiza TPA kuanza kufanya kazi saa 24 kila siku kwa siku saba za wiki ili
kusadia kuongeza ufanisi na kupunguza msongamano wa mizigo
bandarini
Agizo hilo amelitoa leo
jijini Dar es salaam katika ziara fupi bandarini hapo ikwa sambamba na waziri wa
fedha Dk. Wiliam Mgimwa, waziri wa viwanda na biashara Dk. Abdalah Kigoda na
Naibu waziri wa nishati George Simbachawene.
Waziri wa fedha Dk.
Wiliam Mgimwa ametaka mizigo yote inayoingia na kutoka bandarini iwekewe
utaratibu mzuri ili kila mzigo ulipiwe kodi kwa lengo la kuongeza mapato ya
serikali.
Waziri wa viwanda na
biashara Dk. Abdalah Kigoda amesema pamoja na mambo mengine katika kuimarisha
utendaji ndani ya mamlaka hiyo, ameutaka uongozi TPA kuzingatia zaidi maadili,
na pia ameitaka shirika la viwango Tanzania TBS Kufanya kazi masaa 24 kila siku
kwa wiki ili kuongeza ufanisi ndani ya bandari.
Awali akisoma ripoti ya
utendaji Kaimu Mkurugenzi Mkuu TPA Madeni Kipande amesema mamlaka hiyo inahitaji
zaidi ya Dola bilioni 3 kusadia kuimalisha huduma za mamlaka hiyo ikiwemo
uimajishaji wa matumizi ya treni katika usafirishaji wa mizigo kutoka
bandarini.
Post a Comment