Na Cathbert Kajuna, Dar es Salaam
Jeshi la Polisi Tanzania limewakamata zaidi ya
wasichana wapatao 22 eneo la Mwananyamala karibu na geti la Mwananyamala
hospitali akiwemo mama mtu mzima anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 ambaye
alikuwa anamiliki jumba lenye zaidi ya vyumba 40 ambalo utumika kufanyia ukahaba
maarufu kama danguro.
Akitoa taarifa leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kipolisi Kinondoni, Kamanda Charles Kenyela, alisema kuwa wanashukuru wananchi
ambao wameweza kutoa ushirikiano wa kukamatwa kwa wasichana hao ambao walikuwa
wakifanya biashara ya ukahaba katika maeneo hayo kwa muda
mrefu.
Mashuhuda wa tukio hilo, walisema kuwa wanalishukuru
sana Jeshi Polisi kwa kuweza kuwakamata wasichana hao ambao wamekuwa wakifanya
biashara hiyo ya ukahaba kwa muda mrefu.
"Tunalishukuru sana Jeshi la polisi kwa kuvunja kero
hii ambayo imekuwa ikitukera tokea muda mrefu sana, yani danguro hili lipo tokea
mwaka 1990, mimi nazaliwa nalikuta mpaka leo lipo ila leo ndiyo polisi wamekuja
kuwakamata wahusika" Alisema mmoja ya vijana wanaoishi eneo
hilo.
Shuhuda huyo aliongeza kuwa wasichana hao walikuwa
wanafanya biashara hiyo kwa bei ya shilingi 2000, 3000 kwa muda mfupi (short
time) na wateja wao ni vijana, akina baba pamoja na vijana ambao huwa wanabarehe
kwa vile hawa huwa hawajui mapenzi huko huenda kufundishwa.
Post a Comment