Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akipanda treni kishujaa huku mamia ya Watu wakishuhudia na kumshangilia sana.
Katibu Mkuu wa
CCM, Kinana akipunga mkono baada ya kupanda treni kutoka Dar kwenda Kigoma
wakati akiwa na msafara wa viongozi wenzake wakielekea mkoani Kigoma leo kwa
ajili kuhudhuria sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa CCM. Picha na Bashir
Nkoromo
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Asha-Rose Migiro akipunga mkono baada ya
kupanda treni kutoka Dar kwenda Kigoma leo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM ya Wilaya ya Temeke, Emmanuel John hakuwa nyuma kushuhudia tukio la kihistoria la Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akienda kigoma kwa treni pamoja na sekretarieti yake nzima.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisalimiana na mamia ya watu waliofurika stesheni kushuhudia wakienda Kigoma kwa treni
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiwaaga wana Dar Es Salaam muda mchache kabla hajapanda treni kuelekea Kigoma kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM. Wameamua kusafiri kwa treni ili kuwataarifu wadau kuwa usafiri wa treni wa Dar na Kigoma upo imara na wanaiunga mkono serikali kwa jitihada zake za kuifufua reli ya kati.
Baadhi
ya Wana CCM wakimuaga Kinana na msafara wake kutoka stesheni ya reli Dar es
salaam kwenda Kigoma, leo.
Post a Comment