Klabu ya Shanghai Shenhua
imesema kuwa Didier Drogba angali mchezaji wake na kuwa uhamisho wake hadi klabu
ya Galatasaray inakiuka masharti ya mkataba wake.
Mchezaji huyo wa zamani wa
Chelsea, amesaini mkataba wa miezi kumi na minane na klabu ya Galatasaray
inayoshiriki katika ligi kuu ya Uturuki.
”Tumeshangazwa sana na
tangazo hilo” Klabu hiyo ambayo ilimsaini Drogba kwa mkataba wa miaka miwili na
nusu mwezi Julai mwaka uliopita, imesema.
”Drogba angali mchezi wa
klabu ya Shanghai Shenhua kwa kuwa mkataba kati yao bado
haujakamilika.
Klabu ya Galatasaray siku
ya Jumanne ilitangaza kuwa Drogba atajiunga na klabu hiyo baada ya kukamilika na
mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Afrika
Kusini.
Lakini Shenhua imepinga
uhamisha huo na kussema kuwa liko tayari kuwasilisha malalamishi yake ya
shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.
Mchezaji hiyo mwenye umri
wa miaka 34, kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini kuiongoza kikosi cha Ivory Coast
katika mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya
Afrika
Post a Comment