Mamlaka ya mawasiliano
Tanzania TCRA imeyataka makampuni ya simu za mkononi Tanzania kuhakikisha
yanaanza rasmi mpango wa punguzo la bei ya kupiga simu katika mitandao mingine
kutoka bei inayotumika sasa hivi ya shilingi 113 kwa dakika mpaka shilingi 34 na
senti 92 ikiwa ni bei mpya inayotakiwa kuanza kutumika kuanzia siku ya kwanza ya
mwezi March 2013.
Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA
Profesa John Nkoma amesema uamuzi wa kufanya hivyo ni kutokana na kupanda kwa
gharama za maisha ambapo makampuni hayo yanatakiwa kuanza utekelezaji wa agizo
hilo na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa kampuni yeyote ambayo itafanya
kinyume na hayo maagizo.
Namkariri
akisema “bei itaendelea kushuka kadri miaka inavyokwenda, tarehe 1 january 2014
bei itatakiwa kuwa sh 32 na senti 40, tarehe 1 january 2015 sh
30 na senti 58, tarehe 1 january 2016 itatakiwa kuwa sh 28 na senti 57, hizi bei
ni za juu kabisa na Kampuni za simu ni ruksa kwao kuzungumza na wakatumia bei ya
chini kabisa”
Post a Comment