Viongozi wa ngazi ya juu
wa Jeshi la Magereza, ugeni kutoka nchini Vietnam pamoja na wageni mbalimbali
walioalikwa katika sherehe hiyo wakigongesha vinywaji vyao ikiwa ni ishara ya
kufurahi kuwepo pamoja katika eneo hilo.
Rais wa Kiwanda cha
Kutengeneza Kofia ngumu za kisasa (Helmet) kilichopo nchini Vietnam, Greig
Craft (kulia) akimpa zawadi Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja.
Mkuu wa Jeshi la
Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (wa pili kutoka kulia) akitoa
shukrani kwa ugeni kutoka nchini Vietnam kwa kuitikia mwaliko wa kupata chakula
cha jioni. Kulia ni Hoang Thi Na Huong, Naibu Mkurugenzi wa Kiwanda cha
kutengeneza kofia ngumu (Helmet) kilichopo nchini Vietnam. Wa kwanza kushoto ni
Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna Edita Mallya. Anayefuata
ni Rais wa Kiwanda cha Kutengeneza kofia ngumu za kisasa nchini Vietnam, Greig
Craft, na wa katikati ni Gaston Sanga, Kamishna wa Utawala na Fedha wa
Magereza.
Wageni waalikwa
wakishiriki chakula cha jioni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna
Jenerali John Minja.
Mkuu wa Jeshi la
Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (katikati) akimtambulisha Gaston
Sanga, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza kwa ugeni kutoka nchini Vietnam.
Wa pili kutoka kushoto ni Deonice Chamulesile, Kamishna wa Huduma za
Urekebishaji wa Magereza. Ugeni huo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza
wanatarajia kujenga kiwanda cha kofia ngumu za kisasa (Helmet) nchini hivi
karibuni ili kuzuia ajali mbalimbali zinazotokana na
pikipiki.
Mkuu wa Jeshi la
Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akifurahia jambo na Rais wa
Kiwanda cha Kutengeneza kofia ngumu za kisasa nchini Vietnam, Greig
Craft.
PICHA ZOTE
NA
KITENGO CHA MAWASILIANO
YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
YA NCHI
Post a Comment