Msanii wa filamu
nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, leo baada ya Msajili wa Mahakama Kuu kutokuwepo ofisini na hivyo kurudi
rumande hadi kesho tarehe 29/1/2013 atakapoletwa kwa ajili ya kutimiza masharti
ya dhamana ikiwa ni pamoja na kusalimisha kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya
kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa
msajili kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa
serikali ambao watasaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja. Lulu anakabiliwa na
kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
(Picha na Habari Mseto Blog)
Lulu akipanga gari la
magereza.
Lulu akisindikizwa na
askari Magereza.
Lulu akiingia katika
gari la Magereza kwenda Rumande
DAR ES SALAAM,
Tanzania
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo
ilimpatia masharti matano ya kupata dhamana kwa msanii wa Filamu nchini
Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayekabiliwa
na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven
Kanumba.
Masharti hayo yaliyolewa
jana na Jaji Zainabu Mruke muda mfupi baada ya mawakili wa Lulu, Peter Kibatara,
Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe kuiomba mahakama hiyo impatie dhamana
mshtakiwa huyo ambaye anasota rumande tangu April mwaka jana ambapo walieleza
kuwa ombi la dhamana wameliwasilisha chini ya kifungu
cha
148(1) ,(2) Cha Sheria
ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .
Jaji Mruke alisema ili
mahakama impatie dhamana ni lazima asalimishe kwa Msajili wa mahakama hiyo hati
ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama, kuripoti
kwa msajili kila mwezi ,kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa
serikali ambao watasaini bondi ya Sh.milioni 20 kila
mmoja.
Baada ya jaji huyo
kutangaza masharti hayo Lulu na wakili wake walitoka nje ya ukumbi uliokuwa
ukiendeshwa kwa shauri hilo kwa ajili ya kwenda kwa msajili kutimiza masharti
hayo lakini kwa bahati mbaya Msajili hakuwepo ofisini na hivyo kufanya Lulu
kurudishwa rumande hadi leo atakapoletwa kwa ajili ya kujatimiza masharti hayo
mbele ya Msajili wa mahakama hiyo.
Kufuatia mahakama hiyo
jana kumpatia masharti ya dhamana Lulu kutoka na ombi lake Na.125/2012 la kuomba
mahakama hiyo impatie dhamana, lakini bado kesi ya msingi inayomkabili Lulu
ambayo ni ya kuua bila kukusudia bado haijapangiwa jaji wala tarehe ya kuanza
kusikilizwa.
Desemba 21 mwaka jana ,
Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliifunga kesi
ya kuua bila kukusudia Lulu na kuiamishia rasmi kesi hiyo katika Mahakama Kuu,
na uamuzi huo wa mahakama ulitokana na upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya
kesi yake kwa kina mshtakiwa huyo na kuieleza mahakama kuwa wanakusudia kuleta
jumla ya mashahidi tisa.
Post a Comment