Ally Mustafa 'Barthez, na Nizar Khalfani wakifanya mazoezi ya Gym leo asubuhi katika hoteli ya Fame Residence |
Timu ya Young Africans
leo asubuhi imemaliza mazoezi yake kwa kufanya mazoezi ya kujenga mwili na
uimara (Gym) iliyopo katika hoteli ya Fame Residence leo asubuhi na yakiwa ndio
mazoezi ya mwisho katika kambi ya mafunzo ya wiki mbili iliyokuwa ikiendelea
katika viwanja vya Fame Residence Football mijini Antlaya.
Kocha mkuu Ernest Brandts
akishirikiana na Fred Felix Mizniro na Razaki Siwa leo waliongoza mazoezi ya Gym
kuanzia majira ya saa tatu na nusu asubuhi mpaka majira ya saa saa tano na nusu
asubuhi ambapo baada ya mazoezi hayo wachezaji wamepewa nafasi ya kupumzika
kujiandaa na safari ya hapo kesho kurudi Tanzania.
Akiongelea michezo ya
kirafiki mitatu waliocheza na timu za Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen Fc
kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata
nafasi ya kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi
na kuendelea kufanya vizuri.
Tumecheza michezo mitatu,
wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu
yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za mchezo licha ya Arminia kusawaisha
bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa maamuzi sawa na mshika
kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
Mchezo wa pili dhidi ya
Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za
kufunga lakini umakini wa washambuliaji ulitukosesha ushindi kwani Tegete
alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao la mapema kabla ya Waturuki
hawajasawazisha kwa bao la utata kisha kupewa penati ya utata
pia.
Wachezaji wa Young
Africans, Juma Abdul, Said Bahanuzi & Didier wakifanya mazoezi ya Gym leo
asubuhi katika Hotel ya Fame Residence
Mchezo wa mwisho dhidi ya
Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza tuliutawala
mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini wa
washambuliaji wetu pia kulichangia sisi kukosa ushindi, kabla ya kipindi cha
pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo mawili ya haraka haraka kutokana na
uzembe wa walinzi na mlinda mlango Yusuph abDUL
Tunaushukuru uongozi kwa
kukubali kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu
huku tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa na
hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo
yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na
mashindano yatakayotukabili alisema 'Brandts
Post a Comment