MWANAMUZIKI
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jay
Dee, jana alifanikiwa kukamilisha ziara yake ya siku sita ya kupanda mlima
Kilimanjaro, ikiwa na lengo la kutangaza mlima huo na kujionea upekee wa kivutio
hicho.
Katika ziara
hiyo iliyodhaminiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini (TANAPA), msanii huyo
aliyeambatana na mumewe ambaye ndiye anesimamia kazi zake, Gadna Habash,
waliwasili kwenye lango kuu la Marangu saa
12 jioni na
kupokelewa na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA), Erastus
Lufungulo.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kushuka mlimani, Jay Dee,
alisema ziara hiyo imetoa mafunzo makubwa kwao na wakatoa wito kwa wasanii,
waandishi wa habari na watangazaji nchini, kutembelea vivutio hivyo ili kufahamu
yale wanayozungumza kuhusu hifadhi hizo.
“ziara hii
imenipa mwanga kama msanii, nimejifunza mengi na niwakumbushe tu wasanii
wenzangu kuchukulia zoezi la kupanda la kupanda mlima Kilimanjaro kama moja ya
majukumu na wajibu wao kama wananchi wa taifa hili,” alisema
Jide
Kwa upande
wake mhifadhi wa KINAPA Lufungulo ametoa rai kwa wadau wote hasa wananchi wa
kawaida kushiriki kupanda mlima huo, kwa lengo la kukuza utalii wa
ndani.
Post a Comment