Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’
akishuka kutoka katika gari lililomleta leo Mahakama Kuu wakati wa kukamilisha
taratibu za kupata dhamana. (Picha na
Habari Mseto Blog)
Lulu akiingia Mahakamani huku akisindikizwa na
Askari Magereza
Lulu akiingia mahakamani huku akitabasamu.
Lulu akiingia mahakamani.
Lulu akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa
habari waliotala kufanya nae mahojiano mfupi baada ya kupata dhamana.
Lulu akiangua kilio baada ya kushindwa kuongea
na waandishi wa habari waliokusanyika mahakamani hapo.
Lulu akitoka katika lango Kuu la Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam baada ya kupata dhamana.
Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku
nyumba akifuatiwa na mama yake mzazi.
Wasanii nao wallijitokeza mahakamani hapo
kumfariji Lulu, kulia ni msanii wa filamu, Muhsin Awadh 'Dk. Cheni'
Lulu akiondoka mahakama hapo.
Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi
wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, leo. Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili
ambao ni watumishi wa serikali waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila
mmoja, kusalimisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa
ya mahakama na kuripoti kwa msajili kila mwezi. Lulu anakabiliwa na kesi
ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven
Kanumba.
Chanzo: Habari Mseto Blog
Post a Comment