Mabingwa watetezi wa
kombe la mataifa bingwa barani Afrika, Chipolopolo ya Zambia, leo wamebaunduliwa
nje ya mashindano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika baada ya
kutoka sare 0-0 na Burkina Faso katika mechi yao ya mwisho ya
makundi.
Burkina Faso imeanza
mechi hiyo kwa bahati mbaya baada ya nyota wake Alain Traore kupata jeraha na
kuondolewa uwanjani baada ya dakika kumi pekee.
Traore amefunga magoli
matatu zikiwemo mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Ethiopia ambayo walishinda
kwa magoli manne ya yai.
Dakika chache baadaye
Davis Nkausu, wa Zambia vile vile alijeruhiwa na kuondolewa uwanjani na mahala
pake kuchukuliwa na Joseph Musonda baadda ya kugongana na mlinda lango wa
Burkina Faso.
Kufikia wakati wa
mapunziko timu hizo mbili zilikuwa zimetoshana nguvu ya kutofangana bao
lolote.
katika kipindi cha pili
Zambia ilifanya mashambulio kadhaa katika lango la Burkina Faso, lakini juhudi
zao zligonga mwamba.
Mechi hiyo ilimalizika
huku timu hizo mbili zikigawamna alama moja kila moja na hivyo Burkina Faso
kusonga mbele baada ya kukusanya jumla ya alama tano nayo zambia ikiridhika la
alama mbili.
Nigeria imeongoza kundi
hilo kwa jumla ya alama tano huku Ethiopia ikivuta mkia na alama
moja.
Post a Comment