Waziri mstaafu na Mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Job Lusinde akitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (alhamisi januari 24, 2013) ambapo alikutana na wajumbe wa Tume hiyo kutoa maoni na uzoefu wake kuhusu uandishi wa Katiba Mpya. Anayemwongoza ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba na wa kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiagana na Waziri mstaafu na mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Job Lusinde mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yake na Tume hiyo leo (alhamisi januari 24, 2013), ambapo alitoa maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
PICHA NA TUME YA KATIBA
Waziri mstaafu na Mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Ibrahim Kaduma akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yake na Tume hiyo leo (alhamisi januari 24, 2013) ambapo alitoa maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba na kulia ni Mjumbe wa Tume, Profesa Mwesiga Baregu.
Waziri mstaafu na Mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Ibarahim Kaduma akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba mara mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yake na Tume hiyo leo (alhamisi januari 24, 2013) ambapo alitoa maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya. . Mwingine ni Mjumbe wa Tume hiyo, Dkt. Salim Ahmed Salim.
Post a Comment