Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MALI ZA VIGOGO KUHAKIKIWA UPYA

MALI za viongozi 254 zitahakikiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kubaini na kushuhudia kama kweli zinalingana na matamko yao waliyoyajaza katika fomu za tamko la mali na madeni.
Kamishna wa Maadili, Jaji Salome Kaganda alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala.
Jaji Kaganda alisema kuwa, sekretarieti inalazimika kufanya hivyo ili kujiridhisha kama kweli mali zina thamani sawa na matamko waliyoyatoa mwisho wa mwaka jana.
Alisema kuwa, kumekuwapo na changamoto ya baadhi ya viongozi kutoa matamko yanayotofautiana na uhalisia, jambo linaloilazimu sekretarieti hiyo kuhakiki kwa macho uwepo wa mali hizo na maelezo yaliyotolewa.
Jaji Kaganda aliongeza kuwa, Machi 2012, sekretarieti hiyo ilifanya uhakiki kama huo wa mali za viongozi 133 na kubaini upungufu uliojitokeza kutokana na udanganyifu.
Alibainisha kuwa uhakiki huo, ulibaini kuwa kati ya viongozi hao walikuwamo nane ambao walikiuka sheria ya maadili kwa upotoshaji wa mali zao.
Hata hivyo Jaji Kaganda hakuwataja majina viongozi hao, na kusema kuwa bado jambo ilo linaendelea kufuatiliwa kimaadili na sekretarieti hiyo.
Aliongeza kuwa katika viongozi hao waliohakikiwa, sita walibainika kuwa taarifa zao zilikuwa na upungufu na hivyo kutakiwa kuzirekebisha tena.
Alisema kuwa katika uhakiki mpya wa viongozi hao 254, watapitia mali zao walizoziainisha ili kubaini iwapo kuna upungufu au zilijazwa kwa ukweli.

chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top