Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DK SHEIN KUONGOZA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA

 

Shein Pix            Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuongoza Mkutano wa saba wa Baraza la Biashara Zanzibar utakaofanyika Jumamosi Januari 19 katika ukumbi wa Salama Hoteli Bwawani mjini Zanzibar.
 Akitoa taarifa kwa Vyombo vya habari huko Gulioni katika Jengo la ZSTC Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Ali Haji Vuai alisema mkutano huo wa saba utazikutanisha Sekta za Umma na Sekta Binafsi, ambao utajadili mada mbili muhimu ambazo ni Maendeleo ya uwekezaji katika viwanda na Ubiya unaohitajika katika viwanda vya Zanzibar.
Amesema wameamua kuzungumzia masuala hayo kutokana na Sekta ya Viwanda Zanzibar kuwa nyuma sana jambo ambalo pia huchangia ukosefu wa Ajira kwa vijana na mapato kwa maendeleo ya Zanzibar. Ameongeza kuwa Zanzibar ina fursa nzuri ya kuanzisha viwanda vipya na kuvifufua vile vilivyokuwepo awali jambo ambalo litachochea kasi ya maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa Zanzibar.
 Vuai amefahamisha kuwa Viwanda vilivyokufa Zanzibar vilitokana na sababu mbalimbali na kwamba Mkutano huo utakuwa ni sehemu muafaka ya kuelezea chanzo cha kufa viwanda hivyo na kubuni mipango mipya ya kufufua sekta hiyo. Alisema wamealika wadau mbalimbali wa Viwanda na Biashara kutoka ndani na nje ya Zanzibar kuja kujadili namna bora ambapo anaamini kuwa mwisho wa Mkutano huo Zanzibar inaweza kuja na fikra mpya ya juu ya Viwanda.
 Aidha Katibu huyo alisema katika Mkutano huo Makala tatu zitawasilishwa mbili kutoka katika Sekta ya Umma na moja itawasilishwa na Sekta binafsi kuhusiana na mambo yanayohusu njia bora za kuimarisha sekta ya Viwanda Zanzibar. Katibu Vuai pia amewaomba Wajasiriamali wa Zanzibar kuitumia fursa hiyo adhimu kwao kutangaza biashara zao kupitia Wageni na wenyeji ambao watashiriki katika mkutano huo wa Saba toka kuanzishwa Baraza la Biashara la Zanzibar.
 Mkutano huo wa siku moja unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 350 kutoka ndani na nje ya Zanzibar ambapo Mashirika kama UNIDO, TIDO, TMS, Tume ya Biashara ya Afrika ya Mashariki ni miongoni mwa waalikwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top