Mahmoud Ahmad Arusha
Wananchi wenye hasira kali hapa nchini wametakiwa kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuwapiga ama kuwachoma moto watu wanaodaiwa kuwa ni wezi bila ya kujua kama madai wanaotuhumiwa nayo ni ya kweli au la na wengine kujikuta wakipoteza maisha bila ya kuwa na hatia na kutakiwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na usalama.
Kauli hiyo imetolewa na wananchi mbali mbali
wakati wakiongea na waandishi wa habari kwenye matukio mawili tofauti
yaliyotoke kwenye sehemu mbili tofauti kwenye stand kuu ya mabasi na
stand ndogo ya vifodi jijini hapa jana.
Katika tukio la kwanza
kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 37 mkazi wa jijini hapa
mwenye ugonjwa wa akili alipata mkong'oto wa kufa mtu baada ya kupiga
gari la mtu lililokuwa kwenye stand hiyo na kumwaga vyakula na karanga
za wafanyabiashara ndogo ndogo na vijana stand hapo
kumpa mkong'oto huo.
Vijana hao huku wakimpa mkong'oto kijana
huyo walikuwa wakimwambia kuwa wanampa dawa ya sigareti kubwa kwani dawa
yake wanayo wao kijana huyo aliendelea kupatiwa mkong'oto nhadi askari
wa jeshi la polisi aliyekuwa doria stand hapo kumuokoa na kumfikisha
kwenye vyombo vya usalama kumuokoa na kipigo hicho kutoka kwa vijana
wasio na chembe hata ya huruma kwa mgonjwa huyo.
Katika tukio la
pili kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 17 mkazi wa jiji hili
alipata mkong'oto wa paka mwizi hadi kushindwa kujua uelekeo wake wa
kwenda baada ya kudai kuiba vitu kwenye duka moja stand ndogo ya vifodi.
Waandishi
walipohoji kwa mwenye duka hilo ni vitu gani vimeibiwa kwenye duka hilo
alishindwa kuthibitisha kuwa alIIbiwa nini dukani humo huku mgambo wa
jiji wakiangali bila ya kuchukuwa hatua yeyote.
Tarifa zinadai kuwa wananchi mbali mbali wamekuwa wakipatiwa mkong'oto bila ya kuwa na hatia ya makosa wanayotuhumiwa
na kuwataka wananchi mbali mbali kutokujichukulia sheria mikononi
Alipohojiwa
kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas kuhusiana na wananchi
kujichukulia sheria mkononi alisema matukio mengi ya kujichukulia sheria
mkononi ni tatizo hapa nchini huku akiwataka watanzania kujenga mazoea
ya kujichunguza kabla ya kujichukulia sheria mkononi.
Post a Comment