Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MALIM SEIF AKUTANA NA WANDISHI WA HABARI


Makamo wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Malim Seif Sharif Hamad amesema maoni yake juu ya madadiliko ya katiba ni maoni yake binafsi  kama Seif Sharif Hamad na kamwe yasihusishwe na chama chake wala serikali. Amesema maoni hayo hayawakilishi chama wala serikali kwani vyama na serikali vina nafasi yao maalum ya kutoa maoni yao.

Hayo ameyasema leo huko Hoteli ya Bwawani wakati alipo kuwa na mkutano wa pamoja na wandisahi wa habari kuelezea yale aliyoyazungumza  na Tume ya kukusanya maoni  juu ya Katiba mpya  chini ya mwenyekiti wake Joseph Sinde Warioba yaliofanyika nyumbani kwake.

Amesema kama ni mwananchi wa kawaida ameipongeza tume hiyo kwa kuweka utaratibu wa kusikiliza maoni hayo ambayo hapo baadae yatafanyiwa kazi kwa ajili ya kupata katiba ambayo  wananchi wanitaka.

Ameongeza kuwa tume imetoa muongozo ambao wananchi wanaweza kujikita katika   maeneo makuu tisa yalio anishwa na Tume hiyo ambayo ni pamoja na Muundo wa Nchi na Taifa ndani ya Jamhuri ya  MuunganowaTanzania, mamboyenyewe ni HakizaBinadamu na Wajibu wa Wananchi,Ardhi,Maliasili,Mazingira,mihimili yaNchi,Watu,Utawala,Serikali,Bunge, Mahkama,Serikali za Mitaa, Muundo na Mamlaka yake,Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Alisema yanapotazamwa kwa undani maeneo hayo itaonekana kwamba takriban mengi si mambo ya Muungano na hivyo hayawahusu wananchi wa Zanzibar ambao kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano wa 1964 yanasimamiwa na Zanzibar yenyewe ambayo ina mamlaka kamili (exclusive jurisdiction) kuhusiana na mambo yote yasiyo mambo ya Muungano.

Alisema maeneo ambayo yanaweza kuwahusu Wazanzibari kwa mfano misingi na maadili ya kitaifa, madaraka ya wananchi, mihimili ya utawala (Serikali, Bunge na Mahkama) na vyombo vya ulinzi na usalama, kuhusika kwao kutakuwa ni kwa kiasi kile yanapohusika na uendeshaji wa Muungano. “ Ndiyo kusema kwamba jambo lililo katikati ya mjadala kwa Wazanzibari katika mchakato huu ni Muungano wenyewe“alisema Malimu Seif.


Mimi nimeamua kutoa changamoto kupitia waraka huu kwa kuitazama historia ya Muungano, jinsi ulivyoundwa, matatizo yanayoukabili, nafasi na hadhi ya Zanzibar katika Muungano na nini khatima ya Zanzibar na mustakbali wa Muungano katika mchakato huu tunaoendelea nao wa kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano. Nitakayoyaeleza yanaweza yakaonekana ni machungu kwa wakati huu lakini yanaweza yakawa ndiyo ufumbuzi mjarab kwa siku zijazo”.

Malimu seif ali ishukuru tume hiyo kufika kwake na kutoa mchango wake binafsi juu ya mchakato mzima wa ukusanyaji maoni kutafuta katiba mpya ya watanzania ifikapo 2014 mwaka ujao.

Na Mwandishi wetu maelezo Zanzibar 14/1/2013
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top