MWENYEKITI wa NCCR Mageuzi, James Mbatia
---
MWENYEKITI wa NCCR Mageuzi, James Mbatia jana alijikuta katika
wakati mgumu baada ya kulazimika kufungiwa katika ofisi ya NCCR-Mageuzi
wilaya ya Mtwara Mjini kutokana na baadhi wa wananchi walioudhuria
mkutano wake wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa, kutaka kumdhuru
kwa madai kwamba hawakuridhishwa na hotuba yake.
Mbatia alianza kurushiwa chupa tupu za maji
alipokuwa akitoka uwanjani hapo baada ya kukatisha hotuba yake kutokana
na baadhi ya wananchi kupinga kauli zake kwa madai hawamuelewi.
Kauli inayodaiwa kumgharimu Mbatia ni ile ya ‘Iwapo gesi itatoka Mtwara’ ndipo wananchi hao walipoanza kupaza sauti wakisema “Hatukuelewi…hatukuelewi” hata hivyo Mbatia aliendelea kuhutubia hali iliyosababisha wananchi hao wapaze sauti zao kwa kuimba nyimbo.
Kauli inayodaiwa kumgharimu Mbatia ni ile ya ‘Iwapo gesi itatoka Mtwara’ ndipo wananchi hao walipoanza kupaza sauti wakisema “Hatukuelewi…hatukuelewi” hata hivyo Mbatia aliendelea kuhutubia hali iliyosababisha wananchi hao wapaze sauti zao kwa kuimba nyimbo.
“Haitoki… Hatoki…Haitoki…” sauti za wananchi zilisikika na hata
Mbatia alipojaribu kuwatuliza wananchi hao kwa kusema ‘gesi kwanza….
Gesi kwanza” baadhi waliitikia na wengine waliendelea kusema
hawamuelewi.
Hali hiyo ilimlazimisha Mbatia kukatisha hotuba
yake saa 11.25 jioni na aliondoka uwanjani hapo kwa kutembea kwa miguu
hali iliyotoa mwanya kwa wananchi kumrushia chupa tupu za maji.
Mwenyekiti huyo akiwa ameambatana na wabunge wa chama hicho, Moses
Machali (Kasulu Mjini) na Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) mkoani
Kigoma, walielekea kituo cha polisi kilichopi karibu na uwanja huo na
baadaye alielekea ofisi za NCCR Mageuzi wilaya.
Post a Comment