Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAMBO YATAKAYOWEZA KUHARIBU BIASHARA ZAKO

Baadhi ya mambo machache yenye kuharibu biashara zetu.
1. Kushindwa kugawa Madaraka
Kiukweli ingawa mjasiriamali inabidi uwe kila kitu katika biashara yako lakini, kuna ulazima wa kugawa madaraka na majukumu kwa watu wa chini au watu wengine! Kugawa madaraka kutakupa nafasi ya kupumzika pale inapobidi na kuweza kutilia mkazo mambo kwa umakini zaidi.
2. Usilazimishe Kila Maamuzi yapitie Ofisi yako
Kufanya hivi kutapunguza msongamano na lawama zisizo za lazima na kufanya mambo yaende vizuri. Hakuna ulazima wa kila maamuzi yapitie kwako, mengine wewe unapewa taarifa na utendaji ulivyoenda.
3. Kukosa tahthmini na kutafakari ya baadae
Kuna baadhi ya wajasiriamali wanashindwa kufanya tathmini ya taswira ya biashara yao hapo baadae, badala yake wana ng’ang’ana na yaliyopita. Haimaanishi tusiyape kipaumbele yaliyopita, ila tunatakiwa tuyaone kama changamoto katika kufikiria yanayokuja mbele yetu.
4. Kupoteza muda kwenye shuguli zisizo na manufaa.
Mathalani kushinda muda mwingi saana katika Face Book au Mitandao mingine ambayo kwako haina faida kibiashara zaidi ya kukupotezea muda ambao ungeutumia katika uzalishaji mali au kupumzika.
5. Uoga
Uoga katika kufanya maamuzi au kufanya mambo fulani katika uzalishaji mali au maendeleo ya biashara yako. Badala yake “ukahofu” kuwaudhi watu fulani au ukahofia kushindwa au kuanguka.

CHANZO: Wajasiriamali
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top