Kocha Mkuu wa Taifa Stars,
Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia kambini Januari 6 mwaka huu jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
mechi ya mashindano dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka
huu.
Kwa mujibu wa Kocha Kim,
wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma saa 11.30
jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza Januari 7 mwaka
huu.
Wachezaji
walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars,
Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam),
Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin
Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe
(Simba).
Viungo ni
Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha
(Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa
Sugar).
Washambuliaji
ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa
TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim,
benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),
Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa
(Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela
(Mtunza vifaa).
Post a Comment