Mtuhumiwa wa nyara za serekali Peter Laurence mwenye
kofia
katikati
akiwa na maofisa wa jeshi la polisi chini ya ulinzi ,eneo la
kisongo
mtaa wa mateves nje kidogo ya jiji la Arusha baada ya
kukamatwa
na shehena ya nyara za serikali nyumbani kwake.
Miongoni mwa nyara za serekali
zilizokuwazimehifadhiwa kwenye ghala maalumu kwenye nyumba ya mtuhumiwa Peter
Lawrence zikionekana kwenye maboksi tayari kwa kusafirishwa nje ya
nchi.
JESHI
la polisi mkoani Arusha,limekamata shehena kubwa ya nyara mbalimbali za serikali
zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu,eneo la Matevesi Kisongo nje
kidogo ya jiji la Arusha,zikiwa tayari kwa kusafirishwa nje ya
nchi.
Nyara hizo ni pamoja na
Ngozi za Simba,Chui na Mamba ,meno ya Tembo,vichwa vya Nyani,Swala na
Nyati,Pembe za kifaru,na zingine nyingi ambazo jeshi la polisi linaendelea
kuzitambua.
Sambamba na hilo jeshi hilo
limemtia mbaroni mtuhumiwa wa nyara hizo aliyetambulika kwa jina la Peter
Leurence (55)mkazi Ngaramtoni ya chini,ambaye alikuwa akiwa amezihifadhi kwenye
maboksi zaidi ya 20,kwenye nyumba yake iliyopo eneo hilo.
Kwa mujibu wa kamanda wa
polisi mkoni Arusha,Liberatus Sabas tukio la kukamatwa kwa nyara hizo limetokea
jana majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo eneo la kisongo mtaa wa mateves
baada yak upata taarifa kutoka kwa raia wema.
Kamanda Sabas alisema kuwa
baada ya jeshi hilo kupata taarifa za siri majira ya saa 5 asubuhi walifika eneo
la tukio majira ya saa 7 mchana na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa walinzi wa
wanaolinda eneo hilo kwani waliwanyima kuwapa maelekezo ya kumpata mmiliki wa
nyumba hiyo.
Hata hivyo alisema kwamba
askari hao waliamua kumueka chini ya ulinzi kwa kumshurutisha mlinzi mmoja
iliaweze kuwapa ushirikiano ambapo aliwapaita namba za simu na mtuhumiwa
aliwaambia kuwa yupo magugu mkoani Manyara na angefika saa 12 majira ya
jioni.
Taarifa zinadai kuwa baada
ya mtuhumiwa kufika jitihada za kufanya upekuzi zilifanyika chini ya polisi
wenye silaha za moto na walikuta shehena kubwa ya nyara za serekali zilizokuwa
zimahifadhiwa kwenye ghala maalum na kufungwa kwenye mabox teyari kusafirishwa
kwenda kusikojulikana.
Alisema kuwa polisi
waliamua kuweka ulinzi hadi kulipokucha na huku wakiendelea kumshikilia
mtuhumiwa huyo na jeshi hilo linaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo pamoja na
watoto wake wawili waliokutwa wakiishi kwenye nyumba hiyo.
Aidha kamanda Sabas alisema
kuwa kesho yake polisi waliendelea kufanya upekuzi na kubaini mabox zaidi ya 20
yenye nyara mbali mbali miongoni mwa nyara hizo alizitaja kuwa ni Ngozi za
Chui.Simba,Tembo na Mamba pia kulikuwemo vichwa vya nyani,chui,swala nyati,pembe
za faru ,meno ya tembo na nyingine nyingi ikiwemo mfuko wa silaha inayosadikiwa
kuhifadhia silaha.
Kwa mujibu wa kamanda wa
jeshi la polisi mkoani hapa alisema kuwa Watuhumiwa bado wanashikiliwa na jeshi
hilo kwa mahojiano na watafikishwa kwenye mahakama pindi upelelezi wa tukio hilo
utakapo kamilika.


Post a Comment