Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Nguruka Wilayani
Uvinza mkoani Kigoma leo wakati Katibu Huyo na Wajumbe wengine wa Sekretarieti
ya Chama cha Mapinduzi walipotembelea Kijiji hicho na kufanya mkutano na wakazi
wa eneo hilo baada ya kuhudhuria kikao cha ndani cha Siasa Kata ya Nguruka.
Wajumbe hao walipata mapokezi makubwa Kijijini hapo.
Katibu wa Siasa na
Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akicheza na mmoja wa akina mama wa
Kijiji cha Nguruka ambaye alifurahi sana baada ya kumuona ‘live’ Naibu Katibu
Mkuu huyo wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN).
Katibu wa Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye akiwa katika msafara wa mapokezi ya Sekretarieti ya Chama
cha Mapinduzi huku akipiga ngoma kwa umahiri mkubwa na kuwafurahisha wengi.
Kulia ni Mjumbe wa NEC, Asha Baraka.
Wananchi wa
Nguruka wakiwa kando ya barabara kusubiri Msafara wa Sekretarieti ya
CCM.
Katibu wa Siasa na
Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia) akiwa na Mjumbe wa NEC
kutoka Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Asha Baraka ambaye ni mzaliwa wa Nguruka
mkoani humo wakati wa mapokezi ya wajumbe hao wa Sekretarieti.
Katibu wa
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifanya vitu vyake.
Vijana
hawa walikuwa njiani tayari kwa kutoa maelekezo wapi pa
kupita.
Msanii
Umy Wenceslaus maarufu Dokii ambaye amekuwa ni Kada maarufu wa Chama cha
Mapinduzi akitoa burudani kwa wakazi wa Nguruka hii leo. Dokii pia alitoa
burudani katika mkutano Kijiji cha Uvinza.
credits: Father Kidevu
Post a Comment