Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akisani
kitabu cha wageni wakati wa Halfa fupi ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Pugu
Kajiungeni. Kushoto ni Diwani wa kata ya Pugu Kajiungeni Emelda
Samjela.
Diwani wa kata ya Pugu
Kajiungeni Emelda Samjela akizungumza na wakazi wa Kata yake kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry
Silaa.
Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akitoa
taarifa wakati akizindua Mradi wa Maji Pugu Kajiungeni ambapo amesema mradi huo
unatokana na kisima cha maji chenye urefu wa mita 122 toka usawa wa
ardhi.
Mstahiki meya amesema
kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita 60,000 kwa saa.
Ameongeza kuwa mradi huo utakuwa na mtandao wa mabomba wa kilometa 9, vituo 25
vya kuchota maji, nyumba ya pampu, fensi pamoja na uzio.
Aidha amewataka wananchi
wa maeneo husika ya Pugu Kajiungeni ni kuitunza miradi hii na kutoa ushirikiano
kwa wakandarasi ili kuweza kufanikisha malengo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Diwani
wa Kata ya Pugu Emelda Samjela na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kassim
Mjesa na Kulia ni Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd
inayoshughulikia mradi huo Method Mlay.
Pichani Juu na Chini ni
baadhi ya wakazi wa Kata Pugu Kajiungeni watakaofaidika na mradi huo
wakimsikiliza mstahiki Meya Jerry Silaa (hayupo
pichani).
Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akimkabidhi
Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) barua rasmi
ya mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni unaotekelezwa kwa ushirikiano na wahisani
/wafadhili wa Serikali ya Ubelgiji, Umoja wa Ulaya (EU), Serikali ya Tanzania,
Halmashauri ya manispaa ya Ilala na wafadhili wengine mbalimbali. Anyeshuhudia
tukio hilo ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Kassim
Mjesa.
Mkandarasi wa Kampuni ya
Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) akitoa neno la shukrani baada Mstahiki
Meya kumkabidhi barua rasmi ya ujenzi wa mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni na
kuahidi kutoa ajira kwa Vijana wa maeneo ya Pugu kuanza sasa mpaka mradi
utakapokamilika.
Mstahiki Meya Jerry Silaa
akipongezwa na wakazi wa Pugu baada ya kuzindua rasmi mradi wa maji wa Pugu
Kajiungeni ulioanza kubuniwa rasmi mwaka 2011.
Sehemu ya wakazi wa Pugu
Kajiungeni waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo utakaochukua miezi
Sita kukamilika na kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa maeneo
hayo.
Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala Jerry Silaa (wa sita kushoto) akikagua sehemu ya mradi huo kilipojengwa
kisima chenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita elf 60,000 kwa
saa.
Muonekano wa Kisima
hicho.
Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala Jerry Silaa (wa nne kushoto) na Diwani wa Kata ya Pugu Kajiungeni
Emelda Samjela katika picha ya pamoja na viongozi wa kata
hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala Mh. Jerry Silaa akingumza na vyombo vya habari ambapo amesema mradi huo
wa maji wa Pugu Kajiungeni uhahudumiwa na tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa
lita 140,000 lilipo katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto na matenki mnegine ya
maji yenye ujazo wa lita 45,000 na 100,000 ambayo yanapatikana Pugu Kajiungeni
karibu na Zahanati ya Pugu.
Amefafanua kuwa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imechangia kiasi cha Shilingi 378,000,000 na
kiasi kingine kinachobaki kinatolewa na Serikali Kuu pamoja na
wahisani.
Mradi wote utagharimu
kiasi cha shilingi 1,024,000,000/=.
Mwenyekiti wa Serikali za
Mitaa kata ya Pugu Kajiungeni Nuru Daniel akitoa shukrani zake za pekee kwa
Serikali ya awamu na uongozi kwa kutekeleza ilani za Chama ikiwemo kuwapatia
maji wakazi wa Pugu Kajiungeni.
Post a Comment