Na Sabina Chrispine Nabigambo
Serikali ya Jamhuri ya Africa ya Kati na
muungano wa waasi, wanajiandaa kwa mazungumzo ya amani yaliyopangwa kuanza
nchini Gabon siku ya Jumanne ambapo ujumbe wa kwanza uko mbioni kuwasili katika
mji mkuu Libreville.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois
Bozize, AFP PHOTO/ SIA KAMBOU
Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Kati
inataraji kuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo kati ya waasi na Rais Francois Bozize
, mazungumzo ambayo pia yanaungwa mkono na Marekani na Baraza la Usalama la
umoja wa mataifa.
Hapo jana Waasi walifanikiwa kuteka miji miwili
zaidi usiku wa kuamkia Jumamosi, waziri wa utawala wa majimbo Yoshua Binoua
amethibitisha.
Binoua amesema kuwa waasi hao wameteka miji
hiyo iliyoko karibu na mji wa Bambari mji ambao tayari upo chini ya udhibiti wa
waasi wa Seleka jambo linaloashiria nia yao ya kufanya vita hata wakati wa
majadiliano ya amani.
Chanzo:
kiswahili.rfi.fr


Post a Comment