Na Elizabeth
John
SHIRIKISHO la Filamu Tanzania
(TAFF) limekemea baadhi ya wasanii walioonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa
aliyekuwa msanii wa filamu nchini, Juma Kilowoko
‘Sajuki’.
Pia
limesisitiza kuwa msanii atakaeripotiwa katika vyombo vya habari kufanya vitendo
vya utovu wa nidhamu atafungiwa kuigiza.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba alisema amesikitishwa na kitendo cha
wasanii kuacha msiba na kwenda kunywa pombe wakati msiba huo ni wa
dini.
Alisema
baadhi ya wasanii kuonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa marehemu Kanumba na
wengine katika msiba wa Sajuki.
“Nasikitika kuona msanii
hajitambui hata kidogo, yani anaacha msiba anakwenda kunywa pombe tena jirani na
mahala pa msiba, jamani huu msiba ni wa dini, hivyo atakayeripotiwa vibaya
katika misiba TAFF tutamfungia” alisema Mwakifwamba.
Katika
hatua nyingine alisema msiba huo ulitawaliwa na utani hali ya kwamba
umewakutanisha watani wa makabila.
Msiba
huo ulitawaliwa na utani baada ya kuwepo kwa wasanii wachekeshaji kama vile,
Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya fedha, Lucas
Mhuvile ‘Joti’ na wengineo wengi.



Post a Comment